Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 41

Hud 11:41

هود

وَقَالَ ٱرْكَبُوا۟ فِيهَا بِسْمِ ٱللَّهِ مَجْر۪ىٰهَا وَمُرْسَىٰهَآ ۚ إِنَّ رَبِّى لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Na akasema, "Pandeni humo kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na akasema: Pandeni humo kwa Bismillahi, Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [41]

[41] Na baada ya kwisha liweka tayari jahazi Nuhu aliwaambia watu wake: Pandeni humo kwa kujipigia feli njema kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu (kupiga BISMILLAHI) wakati wa kwenda na wakati wa kusimama, na wakati wa kuingia na wakati wa kutoka humo. Na muombeni Mwenyezi Mungu akusameheni kwa madhambi mlio tenda, na akurehemuni. Kwani maghfira na rehema ni katika shani yake Subhanahu wa Taa'la.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nûḥ alisema kuwaambia walioamini pamoja na yeye, «Pandeni kwenye jahazi kwa jina la Allah Mtukufu. Kwa jina la Allah Mtukufu itatembea majini, na kwa jina la Allah Mtukufu itafika mwisho wa kwenda kwake na kutia nanga kwake. Hakika Mola wangu ni Mwingi wa kusamehe dhambi za mwenye kutubia na kurudi Kwake miongoni mwa waja Wake, ni Mwingi wa huruma kwao kwa kutowaadhibu baada ya kutubia».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net