Hud 11:39
هودفَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُّقِيمٌ
Nanyi mtakuja jua ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi, na itakayemteremkia adhabu ya kudumu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nanyi mtakuja jua ni nani itakaye mfikia adhabu ya kumhizi, na itakaye mteremkia adhabu ya kudumu. [39]
[39] Mtakuja jua nani kati yetu atakaye fikiwa na adhabu ya kumdhalilisha, na atafikiwa na adhabu ya kudumu milele katika Akhera!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mtajua hapo, itakapokuja amri ya Allah Mtukufu kwa hilo, ni yupi yule ambaye itamjia, hapa ulimwenguni, adhabu ya Allah Mtukufu yenye kumtweza na itamshukia, huko Akhera, adhabu ya daima isiyokatika.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net