Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 108 · Aya ya 2

Al-Kawthar 108:2

الكوثر

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَٱنْحَرْ

Maana

Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi. [2]

[2] Ilivyo kuwa umepewa hayo, basi dumisha Swala kwa Mola wako Mlezi kwa usafi kabisa, na uchinje dhabihu wako kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa aliyo kupa ya ukarimu, na akakukhusisha wewe khasa kwa kukupa kheri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi, mtakasie Mola wako ibada zako zote, na uchinje mnyama wako kwa ajili Yake, Peke Yake, pamoja na kutaja jina Lake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kawthar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net