Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 106 · Aya ya 4

Quraish 106:4

قريش

ٱلَّذِىٓ أَطْعَمَهُم مِّن جُوعٍ وَءَامَنَهُم مِّنْ خَوْفٍۭ

Maana

Ambaye anawalisha kutokana na njaa, na anawalinda kutokana na hofu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu. [4]

[4] Ambaye anawalisha wasione njaa, na hali wao wamo katika bonde lisio na makulima, na akawalinda na khofu na watu wengine pembezoni mwao wananyakuliwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mola ambaye Amewapa chakula wakati wa njaa kali, na akawapa amani na utulivu dhidi ya hofu iliyokua kubwa sana.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Quraish

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net