Yunus 10:93
يونسوَلَقَدْ بَوَّأْنَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ مُبَوَّأَ صِدْقٍ وَرَزَقْنَـٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ فَمَا ٱخْتَلَفُوا۟ حَتَّىٰ جَآءَهُمُ ٱلْعِلْمُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِى بَيْنَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ فِيمَا كَانُوا۟ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Na hakika tuliwaandalia Wana wa Israili makao mema, na tukawaruzuku katika vitu vizuri. Nao hawakuhitilafiana mpaka ilipowafikia elimu. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitilafiana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika tuliwaweka Wana wa Is raili kikao chema, na tukawaruzuku vitu vizuri. Nao hawakukhitalifiana mpaka ilipo wafikia ilimu. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitalifiana. [93]
[93] Na tuliwaweka vyema Wana wa Israili wakaishi katika nchi nzuri na huku wakiihifadhi Dini yao, nao wako mbali na dhulma iliyo kuwa ikiwapata; riziki na neema zimewajalia. Lakini mara baada ya kuonja neema ya utukufu baada ya unyonge, yaliwasibu maradhi ya kufarikiana. Wakakhitalifiana juu ya kuwa imekwisha bainika kweli na uwongo! Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao Siku ya Kiyama, na atamlipa kila mmoja kwa alilo tenda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika tuliwashukisha Wana wa Isrãîl mashukio mazuri yaliyoteuliwa katika miji ya Shãm na Misri na tukawaruzuku riziki ya halali iliyo nzuri itokanayo na mazuri ya ardhi iliyobarikiwa. Na hawakutafautiana, katika mambo ya Dini yao isipokuwa baada ya kujiwa na ujuzi wa kuwafanya wao wawe pamoja na washikane, miongoni mwao ni yale yaliyomo ndani ya Taurati kuhusu habari ya unabii wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Kwa kweli, Mola wako, ewe Mtume, Atahukumu baina yao Siku ya Kiyama na Atatoa uamuzi katika yale waliokuwa wakitafautiana juu yake kuhusu mambo yako, wapate kuingia wakanushaji Motoni na Waumini Peponi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net