Yunus 10:9
يونسإِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُم بِإِيمَـٰنِهِمْ ۖ تَجْرِى مِن تَحْتِهِمُ ٱلْأَنْهَـٰرُ فِى جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ
Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawaongoa kwa sababu ya Imani yao. Itapita mito kwa chini yao katika Mabustani yenye neema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika walio amini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawaongoa kwa sababu ya Imani yao. Itakuwa inapita mito kati yao katika Mabustani yenye neema. [9]
[9] Hakika walio amini Imani ya kweli kweli, na wakatenda mema katika dunia yao, Mola wao Mlezi atawathibitisha kwenye Uwongofu kwa sababu ya Imani yao, na Siku ya Kiyama atawatia katika Bustani zipitazo mito kati yake, na wataneemeka kwa neema za milele.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika ya wale ambao wamemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafanya mema, Mola wao Atawaonesha njia ya Pepo na Atawaafikia kufanya matendo yenye kuwafikisha kwake, kwa sababu ya Imani yao, kisha Atawapa malipo mema kwa kuingia Peponi na kuwashushia wao radhi Zake; chini ya sebule zao na majumba yao itakuwa ikipita mito, wakiwa ndani ya mabustani ya Pepo ya starehe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net