Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamtatulia yeye tatizo katika matatizo ya siku ya Kiyama, na atakayemfanyia wepesi mwenye ugumu (katika jambo lake) Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi duniani na Akhera, na atakayemsitiri muislamu Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera, na Mwenyezi Mungu humsaidia mja pale mja anapokuwa katika kumsaidia ndugu yake, na atakayeshika njia akitafuta ndani yake elimu, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kupitia njia hiyo njia ya kuingia peponi, na hawajawahi kukusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakisomeshana baina yao, isipokuwa huwashukia utulivu na huwagubika rehema na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwataja (vizuri) kwa wale walioko kwake (Malaika), na yeyote ambaye matendo yake yatamchelewesha kuingia peponi basi ukoo wake hautompeleka mbio (kuingia)".
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.