Imepokelewa kutoka kwa Abii Dharri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hicho chombo cha Birika kiko vipi? Akasema: "Namuapa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, kwa hakika vyombo vyake ni vingi kama wingi wa nyota mbinguni na sayari zake eleweni vyema kuwa kung'aa kwake kutakuwa katika usiku usio na mwezi, pako safi, vyombo vya peponi atakaye kunywa katika vyombo hivyo hatopatwa na kiu milele wala kiu hakitomrudia, na maji hayo yanaruka na kububujika kupitia mabomba mawili yaliyo juu ya peponi, yeyote atakaye kunywa katika Birika hilo hatopatwa na kiu, upana wake ni sawa na urefu wake ambao ni sawa kutoka Amman mpaka Aila (Ni katika miji ya Jordan, baina yake ni km 330) maji yake ni meupe mno kuliko maziwa, na ni matamu kuliko asali."
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.