Kutoka kwa Uqba bin Amir, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, amesema: “Tulikuwa na zamu ya kuchunga ngamia, basi ikafika zamu yangu nikawapeleka jioni, nikamkuta Mtume rehema na amni ziwe juu yake akiwa amesimama akiwahadithia watu, nikamkuta akiwa katika kauli yake: “Hakuna Muislamu anayetawadha na akautia vizuri udhu wake, kisha akasimama na kuswali rakaa mbili, akielekea kwa moyo wake na uso wake ndani ya rakaa hizo, isipokuwa Pepo itastahiki kwake.” Akasema, nikasema: Ni kheri iliyoje hii, mara ghafla nikasikia msemaji mmoja mbele yangu akisema: Ile ya kabla yake ndio ilikuwa bora, basi nikatazama, mara nikamuona ni Omari, akasema: Nimekuona umekuja hivi karibuni, akasema: “Hakuna yeyote kati yenu atakayetawadha vizuri - au akaukamilisha vizuri- kisha akasema: Nashuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, isipokuwa atafunguliwa milango minane ya Pepo, aingie mlango wowote autakao".
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.