Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake walisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamechukua malipo mengi wenye utajiri: Wanaswali kama tunavyoswali na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka katika mali yao ya akiba. Akasema: Hivi kwani hajakuwekeeni Mwenyezi Mungu mambo mnayoweza kutoa sadaka: Hakika katika kila tasbihi (kauli ya sub-haanallaah) ni sadaka, na kila takbira (Allahu Akbaru) ni sadaka, na kila tahmidi (Alhamdulillah) ni sadaka, na kila tahalili (Laa ilaaha illallaahu) ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka, na katika kiungo cha siri cha mmoja wenu kuna sadaka" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi yawezekanaje akidhi mmoja wetu matamanio yake kisha awe na malipo? Akasema: Mnasemaje ikiwa atakiweka katika haramu, je atakuwa na mzigo wa dhambi? basi ndivyo hivyo akikiweka katika halali atakuwa na malipo".
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.