Imepokelewa Kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- yakwamba yeye alimsikia mtu mmoja akisema: Hapana! naiapia Al-ka'aba, akasema bin Omar: Hakuapiwi kinyume na Mwenyezi Mungu, kwani mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atayeapa kinyume na Mwenyezi Mungu basi atakuwa amekufuru au kafanya ushirikina"
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na majina yake na sifa zake basi atakuwa kamkufuru Mwenyezi Mungu au kafanya ushirikina; kwa sababu kiapo humaanisha kutukuzwa mwenye kuapiwa, na utukufu ni wa Allah pekee; hakuapiwi ila kwa Allah na majina yake na sifa zake kutakasika machafu ni kwake. Na kiapo hiki ni katika shirki ndogo; lakini ikiwa muapaji atakitukuza alichokiapia kama anavyomtukuza Allah Mtukufu au zaidi; basi hapo itakuwa katika ushirikina mkubwa.
Mafunzo
Nikuwa kutukuza kwa kiapo ni katika haki za Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- hakuapiwi ila kwa Allah na majina yake na sifa zake.
Pupa ya Masahaba katika kuamrisha mema na kukataza maovu, hasa hasa uovu unapokuwa unahusiana na ushirikina mkubwa au kufuru.
Marejeo
سنن الترمذي (3/ 194) (1535).
سنن أبي داود (5/ 154- 155) (3251).
مسند أحمد (9/ 249) (5346)، (9/ 275) (5375)، (10/ 249) (6072).
فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، لعبد الرحمن التميمي (ص413).
القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (2/ 214).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص326).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص365).
التمهيد لشرح كتاب التوحيد، لصالح آل الشيخ (ص452).
فتاوى اللجنة الدائمة، (1/ 343).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com