Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Karama za Mawalii.

Hadithi 2

Watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo (vijana), wenye mawazo ya kipumbavu, watazungumza maneno mazuri kuliko maneno ya viumbe wote, (lakini) wanatoka katika Uislamu kama unavyotoka mshale katika upinde

عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: إِذَا حَدَّثْتُكُمْ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَلَأَنْ أَخِرَّ مِنَ السَّمَاءِ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أَكْذِبَ عَلَيْهِ، وَإِذَا حَدَّثْتُكُمْ فِيمَا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ فَإِنَّ الحَرْبَ خَدْعَةٌ، سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «يَأْتِي فِي آخِرِ الزَّمَانِ قَوْمٌ حُدَثَاءُ الأَسْنَانِ سُفَهَاءُ الأَحْلاَمِ، يَقُولُونَ مِنْ خَيْرِ قَوْلِ البَرِيَّةِ، يَمْرُقُونَ مِنَ الإِسْلاَمِ كَمَا يَمْرُقُ السَّهْمُ مِنَ الرَّمِيَّةِ، لاَ يُجَاوِزُ إِيمَانُهُمْ حَنَاجِرَهُمْ، فَأَيْنَمَا لَقِيتُمُوهُمْ فَاقْتُلُوهُمْ، فَإِنَّ قَتْلَهُمْ أَجْرٌ لِمَنْ قَتَلَهُمْ يَوْمَ القِيَامَةِ».
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake: Nikikuhadithieni kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi kuporomoka kutoka mbinguni ni bora zaidi kwangu kuliko kumsemea uongo, na nikikuhadithieni katika yale yaliko baina yangu na nyinyi basi tambueni kuwa vita ni ulaghai (uongo), nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo (vijana), wenye mawazo ya kipumbavu, watazungumza maneno mazuri kuliko maneno ya viumbe wote, (lakini) wanatoka katika Uislamu kama unavyotoka mshale katika upinde, imani yao haitovuka koromeo zao, mahali popote mtakapokutana nao basi wauweni, kwani kuwaua kwao kuna malipo siku ya Kiyama kwa atakayewaua".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba, mtakaponisikia ninakuhadithieni kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi hakika mimi sifichi wala sibuni, wala sifuniki haki, bali ninaweka wazi, na kuanguka kwangu kutoka juu mbinguni ni rahisi na ni bora sana kwangu kuliko kusimulia jambo la uongo nikasema kuwa limetoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na nikisimulia mambo yalio kati yangu mimi na watu wengine, basi vita ni udanganyifu, hapo ninaweza kusema kwa mafumbo au kubuni au kuficha, kwani nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Watatokea katika zama za mwisho vijana wenye umri mdogo, wasiojitambua (madhaifu wa akili) watakuwa wakisema maneno kutoka ndani ya Qur'ani na wakiisoma kwa wingi, watakuwa wakitoka ndani ya Uislamu na wakivuka mipaka yake, kama mshale utokavyo katika upinde, Imani yao haivuki koromeo zao, mahali popote mtakapokutana nao basi wauweni, kwani kuwaua kwao kuna malipo kwa atakayewauwa, siku ya Kiyama.

Mafunzo
  1. Hapa kumebainishwa sifa miongoni mwa sifa za Makhawariji (wanao asi tawala zao).
  2. Katika hadithi hii kuna alama miongoni mwa alama za unabii, kiasi ambacho ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo yatakayotokea baada yake ndani ya Umma wake, na imetokea kama alivyoeleza.
  3. Kufaa kuleta mafumbo na hadaa katika vita, na udanganyifu katika vita unakuwa kwa mafumbo, na unakuwa kwa kuficha, na mfano wake, pasina kuvunja ahadi na amani, kwa kuja kwa katazo katika hilo.
  4. Amesema Nawawi katika neno "Wanazungumza kwa maneno bora kuliko yote" Maana yake: Inavyoonekana ni kama kauli yao: Hakuna hukumu isipokuwa hukumu ya Mwenyezi Mungu, na mfano wa hilo katika madai yao ya kuwaleta watu katika kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  5. Amesema bin Hajari katika kauli yake: "Haivuki imani yao koromeo zao": Makusudio yake nikuwa imani haijakita ndani ya nyoyo zao; kwa sababu kinachosimama katika koo bila kuvuka hakifiki ndani ya moyo.
  6. Amesema Kadhi: Wamekubaliana wanachuoni wote kuwa Makhawariji na mfano wao ni katika watu wazushi na waovu, wakati wowote watakapotoka kwa kiongozi na wakaenda kinyume na mtazamo wa watu wengi, na wakapasua umoja, basi ni wajibu kupigana nao baada ya kuwaonya, na kuwapa udhuru.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 200) (3611). صحيح مسلم (2/ 746) (1066). النهاية في غريب الحديث والأثر (259)(866). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (20/ 264) (20/ 258). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (6/ 58).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Karne bora ni karne yangu, kisha wale wanaowafuata, kisha wale wanaowafuata

عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «خَيْرُكُمْ قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ» قَالَ عِمْرَانُ: لاَ أَدْرِي أَذَكَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعْدُ قَرْنَيْنِ أَوْ ثَلاَثَةً، قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ بَعْدَكُمْ قَوْمًا يَخُونُونَ وَلاَ يُؤْتَمَنُونَ، وَيَشْهَدُونَ وَلاَ يُسْتَشْهَدُونَ، وَيَنْذِرُونَ وَلاَ يَفُونَ، وَيَظْهَرُ فِيهِمُ السِّمَنُ».
Kutoka kwa Imrani bin Huswain radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Karne bora ni karne yangu, kisha wale wanaowafuata, kisha wale wanaowafuata" Amesema Imrani: Sijui alitaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadaye karne mbili au tatu, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika baada yenu kutakuja watu wanaofanya hiyana na wala hawaaminiwi, na wanatoa ushahidi na wala hawatakwi ushahidi, na wanatoa nadhiri na wala hawatimizi, na utadhihiri kwao unene".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa tabaka bora la watu waliokusanyika katika zama moja ni tabaka ambalo yuko ndani yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Maswahaba zake, kisha wale wanaowafuata katika waumini wale waliowapata Maswahaba na hawakumpata Mtume wa Mwenyezi Mungu, kisha wale wanaowafuata nao ni wafuasi wa wanafunzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akapata wasi wasi swahaba katika kutaja wale wanaowafuata kwa karne ya nne. Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika baada yao kuna kizazi (kaumu) watafanya hiyana na wala watu hawatowaamini, na watatoa ushahidi kabla ya kutakwa kutoa ushahidi, na wanatoa nadhiri na wala hawatimizi, na wanachupa mipaka katika ulaji na unywaji mpaka unadhihiri kwao unene.

Mafunzo
  1. Karne na kizazi bora katika umri wote wa dunia ni karne aliyoishi Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Maswahaba zake, na imekuja katika Sahihi Bukhari kutoka kwake rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Nimetumwa katika karne bora zaidi za watoto wa Adam karne moja baada ya nyingine, mpaka nikawa katika karne niliyopo ndani yake".
  2. Amesema bin Hajari: Na hadithi hii imepelekea Maswahaba kuwa bora zaidi kuliko wanafunzi wao (Matabii), na Matabii kuwa bora kuliko wanafunzi wao (Mataabii Taabiina), lakini je, ubora huu ni kulingana na ujumla wao au mtu mmoja mmoja? Hapa ni mahala pa kufanya utafiti, na kwa kauli hiyo ya pili ndio iliyochaguliwa na jopo la wanachuoni.
  3. Ishara ya ulazima wa kufuata njia ya karne tatu za mwanzo; kwani kila ambaye zama zake zitakuwa karibu zaidi na zama za utume basi huyo ndiye anastahiki zaidi kuwa na fadhila na elimu na kuiga na kuongoka kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  4. Nadhiri: Ni mtu mwenye ulazima wa kutekeleza sheria kuilazimisha nafsi yake kwa ibada ambayo sheria haikuifanya kuwa lazima kwa kila kauli iliyoielezea.
  5. Ubaya wa hiyana na kutotimiza nadhiri na kufungamana na dunia.
  6. Ubaya wa kutoa ushahidi pasina kutakwa kuutoa, ikiwa mwenye haki analijua hilo, na ama akiwa hajui linaingia katika kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Hivi je nisikuelezeni mashahidi bora kuliko wote, ni yule anayetoa ushahidi kabla hajaulizwa" Kaipokea Muslim.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 171) (2651). صحيح مسلم (4/ 1964) (2535)، (3/ 1344) (1719). النهاية في غريب الحديث والأثر (747). نيل الأوطار (8/ 341).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com