عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «خَيْرُ يَوْمٍ طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ يَوْمُ الْجُمُعَةِ، فِيهِ خُلِقَ آدَمُ، وَفِيهِ أُدْخِلَ الْجَنَّةَ، وَفِيهِ أُخْرِجَ مِنْهَا، وَلَا تَقُومُ السَّاعَةُ إِلَّا فِي يَوْمِ الْجُمُعَةِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: “Siku bora zaidi iliyochomozewa jua ni siku ya Ijumaa, ndani yake aliumbwa Adam, na ndani yake aliingizwa Peponi, na ndani ya siku hii akatolewa humo, na hakitosimama Kiyama ila siku ya Ijumaa".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake anatueleza kuwa siku bora kabisa iliyochomozewa na jua ni Ijumaa, Miongoni mwa sifa zake: Mwenyezi Mungu alimuumba Adam, amani imshukie, na ndani yake akamuingiza Peponi, na ndani yake akamtoa na akamteremsha duniani, na Kiyama hakitosimama ila siku ya Ijumaa.
Mafunzo
- Ubora wa siku ya Ijumaa kwa siku zingine za wiki.
- Himizo la kukithirisha amali njema siku ya Ijumaa, na kujiweka tayari kwa ajili ya kupata rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuzuia adhabu zake.
- Sifa hizi za siku ya Ijumaa zilizotajwa katika Hadithi zilisemekana kuwa ni kutotaja fadhila ya Ijumaa; Kwa sababu kutolewa Adam peponi na kusimama Kiyama hakuzingatiwi kuwa ni neema, na imesemekana: Bali yote hayo ni neema, na kutoka kwa Adam peponi ndio sababu ya kuwepo kizazi wakiwemo Mitume na Manabii na watu wema, na kusimama kwa Kiyama ndio sababu ya kuharakishwa malipo ya watu wema na kupata yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu miongoni mwa takrima.
- Sifa nyingine za ijumaa zilitajwa zaidi ya hizo zilizotajwa katika riwaya hii, ni pamoja na: ndani yake Adam alitubia, na ndani yake alifishwa, na ndani yake kuna saa ambayo hakuna mja Muumini atakaye afikiana nayo akiwa anaswali na kumuomba Mwenyezi Mungu jambo lolote isipokuwa humpa hilo analoomba.
- Siku bora ya mwaka ni Siku ya Arafa, na inasemekana: Ni siku ya kuchinja, siku bora ya wiki ni Ijumaa, na usiku bora ni Laylatul-Qadri (Usiku wenye cheo).
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 585) (854).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 313).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 824).
مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعبيد الله المباركفوري (4/ 422).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 164).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «دَعُونِي مَا تَرَكْتُكُمْ، إِنَّمَا هَلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ بِسُؤَالِهِمْ وَاخْتِلَافِهِمْ عَلَى أَنْبِيَائِهِمْ، فَإِذَا نَهَيْتُكُمْ عَنْ شَيْءٍ فَاجْتَنِبُوهُ، وَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِأَمْرٍ فَأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu ya maswali mengi na kuwapinga mitume wao, hivyo, nikiwakatazeni jambo basi liepukeni, na nikiwaamrisha jambo lifanyeni kadiri muwezavyo"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hukumu za kisheria zimegawanyika sehemu tatu: Zilizonyamaziwa, na makatazo, na maamrisho.
Ama ya kwanza: Nayo ni ile ambayo sheria imeinyamazia: Kiasi kwamba hakuna hukumu, nakuwa asili ya mambo huwasiyo wajibu kuyafanya; Ama katika zama zake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, ilikuwa ni lazima kujiepusha na kuuliza juu ya jambo ambalo halijatokea kwa kuhofia kuwekewa faradhi au katazo, kwani Mwenyezi Mungu aliliacha kwa ajili ya rehema kwa waja wake, na ama baada ya kufa kwake rehema na amani za Allah zimshukie, ikiwa swali liko katika mfumo wa fatwa au kujifunza kwa yale anayoyahitaji kuhusiana na mambo ya dini basi inajuzu bali imeamrishwa kufanya hivyo, na ikiwa ni katika namna ya jeuri na kuchimbua mambo, basi haya ndio maswali yanayokusudiwa kujiepusha nayo katika Hadithi hii. Na hii ni kwa sababu huenda ikapelekea katika yale yaliyowapata Wana wa Israeli, pale walipoamrishwa kuchinja ng'ombe yeyote lau wangelichinja ng'ombe yeyote basi wangelikuwa wametekeleza amri, lakini walitia mkazo, wakakaziwa pia.
Ya pili: Ni makatazo; nayo ni yale anayopata malipo mwenye kuyaacha, na anaadhibiwa mwenye kuyafanya, ni wajibu kuyaepeuka yote.
Ya tatu: Ni maamrisho; nayo ni yale anayopata malipo mwenye kuyafanya, na anaadhiwa mwenye kuyaacha, hivyo ni wajibu kuyafanya kwa kadiri ya uwezo.
Mafunzo
- Tunapaswa kuzingatia kile ambacho ni muhimu zaidi na kinachohitajika, na kuacha kile kisichohitajika mara moja, na tusijishughulishe na kuuliza juu ya kile ambacho hakijatokea.
- Ni haramu kuuliza maswali ambayo yanaweza kutatiza baadhi ya mambo, na kufungua mlango wa shaka ambayo husababisha kuhitilafiana kwingi.
- Amri ya kuacha makatazo yote; Kwa sababu hakuna ugumu katika kuyaacha, na ndiyo maana katazo lilikuja kwa ujumla.
- Amri ya kufanya kile kilichoamrishwa ni kwa kadiri ya uwezo; Kwa sababu mtu inaweza kuwa vigumu kwake kuitekeleza au akashindwa kuifanya; ndio maana amri ilikuja kuwa ifanyike kwa kadiri ya uwezo.
- Katazo la kuuliza maswali mengi Wanachuoni wamegawanya kuuliza katika sehemu mbili: Moja wapo: Ni maswali yanayokuwa katika mfumo wa kujifunza yale anayoyahitajia mtu kuhusiana na mambo ya dini, hili limeamrishwa, na miongoni mwa aina hii ni maswali ya Maswahaba, na aina ya pili: Ni maswali yanayokuwa katika sura ya kiburi na kujikalifisha, na hii ndiyo iliyoharamishwa.
- Tahadhari kwa Umma huu dhidi ya kumpinga Nabii wake, kama ilivyotokea katika Umma zilizokuwa kabla yake.
- Maswali mengi juu ya mambo yasiyohitajika na kutofautiana na mitume ni sababu ya maangamizo, na hasa katika mambo ambayo hayawezi kufikiwa, kama vile: Masuala ya ghaibu ambayo Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeyajua, na hali za Siku ya Kiyama.
- Katazo la kuuliza maswali katika mambo magumu, amesema Auzaai: Hakika Mwenyezi Mungu akitaka kumnyima mja wake baraka ya elimu, anaweka upotovu katika ulimi wake, na niliwaona watu wa namna hivyo kuwa ni watu wasio na elimu, na amesema bin Wahabi: Nilimsikia Maliki akisema: Mijadala tasa katika elimu hunaondoa nuru ya elimu katika moyo wa mtu.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 94) (7288).
صحيح مسلم (2/ 975) (1337).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 236).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 181).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 268).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمْ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا، فَيَكْسِرَ الصَّلِيبَ، وَيَقْتُلَ الخِنْزِيرَ، وَيَضَعَ الجِزْيَةَ، وَيَفِيضَ المَالُ حَتَّى لاَ يَقْبَلَهُ أَحَدٌ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya ukaribu wa kuteremka Issa mwana wa Mariam amani iwe juu yake ili ahukumu baina ya watu kwa uadilifu na kwa sheria ya Muhammadi. nakuwa atavunja misalaba wanayoitukuza wakristo, nakuwa Issa amani iwe juu yake ataua nguruwe, Na pia amani iwe juu yake ataweka kodi (Jizia) na atawaamrisha watu wote kuingia katika Uislamu. Nakuwa mali itaenea na hatoikubali yeyote; na hii ni kwa sababu ya wingi wake, na kwa kutosheka kila mmoja na kile anachokimiliki mkononi mwake, na kuteremka kwa baraka na heri nyingi zenye kufuatana.
Mafunzo
- Kumethibitishwa kuteremka kwa Issa amani iwe juu yake zama za mwisho, nakuwa tukio hilo ni katika alama za Kiyama.
- Sheria ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haitofutwa na sheria yoyote.
- Kuteremka kwa baraka katika mali zama za mwisho, na watu kutoipenda.
- Habari njema ya kubakia kwa dini ya Uislamu kiasi ambacho Issa amani iwe juu yake atawahukumu watu zama za mwisho.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 82) (2222)، صحيح مسلم (1/ 135) (155)، شرح النووي على مسلم (1/471)، التوضيح (14/555)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (12/ 35).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ صَخْرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْت رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم يَقُولُ: «مَا نَهَيْتُكُمْ عَنْهُ فَاجْتَنِبُوهُ، وَمَا أَمَرْتُكُمْ بِهِ فَافْعَلُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ، فَإِنَّمَا أَهْلَكَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ كَثْرَةُ مَسَائِلِهِمْ، وَاخْتِلَافُهُمْ عَلَى أَنْبِيَائِهِمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira Abdul-Rahman bin Swakhar -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Yale niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi fanyeni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao".
Imepokelewa na Bukhari na MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ametubainishia sisi Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa atakapotukataza kitu basi ni wajibu juu yetu kukiacha pasina kubagua, na atakapotuamrisha kwa chochote basi ni juu yetu kukifanya kile tunachokiweza. Kisha akatutahadharisha ili tusije kuwa kama baadhi ya umma zilizopita pindi walipokithirisha maswali juu ya Manabii wao ikiwa ni pamoja na kwenda kinyume nao, basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa aina mbali mbali za maangamivu na uharibifu, tunatakiwa tusiwe mfano wao ili tusiangamie kama walivyoangamia.
Mafunzo
- Hadithi ni kanuni katika kubainisha kuwa la wajibu ni kutekeleza amri na kujiepusha na makatazo.
- Katazo halikuruhusu kufanya chochote katika hayo, lakini amri imewekwa sharti la uwezo; kwa sababu kuacha ni jambo liko ndani ya uwezo na kufanya kunahitaji uwezo wa kuleta kitendo kilichoamrishwa.
- Katazo la kuuliza maswali mengi Wanachuoni wamegawanya kuuliza katika sehemu mbili: Moja wapo: Ni maswali yanayokuwa katika mfumo wa kujifunza yale anayoyahitajia mtu kuhusiana na mambo ya dini, hili limeamrishwa, na miongoni mwa aina hii ni maswali ya Maswahaba, na aina ya pili: Ni maswali yanayokuwa katika sura ya kiburi na kujikalifisha, na hii ndiyo iliyoharamishwa.
- Tahadhari kwa Umma huu dhidi ya kumpinga Nabii wake, kama ilivyotokea katika Umma zilizokuwa kabla yake.
- Makatazo yanakusanya kidogo na mengi; kwa sababu haiwezekani kuyaepuka ila kwa kuyaepuka kidogo yake na mengi yake, kwa mfano: Ametukataza riba hii inakusanya ndogo yake na kubwa yake.
- Kuacha sababu zinazopelekea katika haramu; kwa sababu hilo ni miongoni mwa maana za kuepeuka.
- Haitakiwi kwa mtu atakaposikia amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake aseme: Je ni wajibu au ni sunna?, bali anawajibika kwenda mbio kutekeleza; kwa kauli yake: "Yafanyeni katika hayo kadiri muwezavyo".
- Wingi wa maswali ni sababu ya kuangamia hasa hasa katika mambo ambayo haiwezekani kuyafikia, mfano kama mambo ya ghaibu, na namna ya hali ya siku ya Kiyama, usizidishe maswali ndani yake utaangamia, na ukawa ni king'ang'anizi na mtafuta mambo kwa undani.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 94) (7288).
صحيح مسلم (2/ 975) (1337).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 236).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 181).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 268).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com