Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Matamko ya Talaka.

Hadithi 1

Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao, madamu hayajafanyiwa kazi au kuzungumzwa

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ عَنْ أُمَّتِي مَا حَدَّثَتْ بِهِ أَنْفُسَهَا، مَا لَمْ تَعْمَلْ أَوْ تَتَكَلَّمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao, madamu hayajafanyiwa kazi au kuzungumzwa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Muislamu haadhibiwi kwa mazungumzo ya shari ya nafsi yake kabla ya kuyafanyia kazi au kuyazungumza, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu ameondolea uzito na kusamehe, na hakuuandikia makosa umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake kwa yale yanayopatikana akilini na yakazunguka katika nafsi bila ya kutulizana nafsi katika hiyo; yakitulizana katika moyo wake, mfano kama kiburi na kujiona au unafiki, au akafanya kwa viungo vyake au akasema kwa ulimi wake basi hapa atahesabiwa.

Mafunzo
  1. Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, ameyaacha na kuyasamehe mawazo na fikira zinazojitokeza katika nafsi, mtu huzungumza mwenyewe ndani ya moyo wake na kupita katika mawazo yake.
  2. Mtu atakapofikiria talaka, na ikapita akilini mwake, lakini akawa hajaitamka na wala hajaiandika, basi hiyo haizingatiwi kuwa ni talaka.
  3. Mazungumzo ya nafsi mtu hahesabiwi vyovyote vile yatakavyokuwa makubwa madam hayajakita ndani ya nafsi yake na akayafanyia kazi au kuyazungumza.
  4. Ukubwa wa cheo cha umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake kwa kufanywa maalum kwa kutokuadhibiwa kwa mazungumzo ya nafsi, kinyume na umma zilizokuwa kabla yetu.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 46) (5269). صحيح مسلم (1/ 116) (127). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (7/ 560). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 46). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (5/ 502). حاشية السندي على سنن ابن ماجه، للسندي (6/ 157). البدرُ التمام شرح بلوغ المرام، للمغربي (8/ 49).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com