Atakayemuua aliyechukua ahadi ya kulindwa, hatonusa harufu ya pepo, na hakika hurufu yake hupatikana kuanzia mwendo wa miaka arobaini
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tahadhari kubwa kwa atakayemuuwa aliyechukua ahadi ya kulindwa -Naye ni kafiri aliyeingia katika mji wa kiislamu kwa ahadi na amani- kuwa hatonusa harufu ya Pepo, na hakika harufu yake huwa kuanzia umbali wa mwendo wa miaka arobaini.
- Uharamu wa kumuua aliyechukua ahadi ya amani na kafiri anayeishi na waislamu, na aliyeomba amani katika makafiri, nakuwa jambo hilo ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.
- Aliyechukua ahadi: Ni kafiri aliyechukua ahadi ya kutowapiga vita waislamu na huku akiishi katika mji wake, na wao wasimpige vita, na dhimi: Ni yule anayeishi mji wa waislamu na akalipa jizia (kodi ya kichwa), na muomba amani: Ni mtu aliyeingia mji wa waislamu kwa mkataba na amani kwa muda maalumu.
- Tahadhari ya kufanya hiyana katika makubaliano na wasiokuwa waislamu.
صحيح البخاري منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 232). توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام، للبسام (6/ 90). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 520). سبل السلام، لمحمد الصنعاني (2/ 501).