Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hukumu na Maswala ya Jihadi.

Hadithi 1

Hakuwahi kuwapiga vita Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu hata siku moja isipokuwa kwanza alianza kuwaita katika Uislamu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا قَالَ: مَا قَاتَلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَوْمًا قَطُّ حَتَّى يَدْعُوَهُمْ.
Kutoka kwa bin Abbas- radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Hakuwahi kuwapiga vita Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu hata siku moja isipokuwa kwanza alianza kuwaita katika Uislamu.
Imepokelewa na Ahmad na AlbayhaqyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yao kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwahi kuanza kuwapiga vita watu mpaka kwanza awaite katika Uislamu, wasipokubali wito wake anawapiga vita.

Mafunzo
  1. Sharti la kufikisha ujumbe wa Uislamu kwanza kabla ya vita, ikiwa Uislamu haujawafikia.
  2. Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwaita katika Uislamu, wakikataa basi anawapa hiari ya kulipa kodi, wakikataa anawapiga vita, kama ilivyokuja katika hadithi zingine.
  3. Lengo la Jihadi ni watu kuingia katika Uislamu, na si tamaa ya kuwaua na kuchukua mali zao na miji yao.
Marejeo

مسند أحمد (4/ 16) (2105). السنن الكبرى للبيهقي (9/ 181) (18232). تحفة الأحوذي (5/ 130).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com