Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Fadhila za Hijjah na Umra.

Hadithi 4

Basi itakapokuja Ramadhani, basi fanya Umra, kwani Umra ndani ya Ramadhani ni sawa na Hija.”

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِامْرَأَةٍ مِنَ الْأَنْصَارِ سَمَّاهَا ابْنُ عَبَّاسٍ فَنَسِيتُ اسْمَهَا: «مَا مَنَعَكِ أَنْ تَحُجِّي مَعَنَا؟» قَالَتْ: لَمْ يَكُنْ لَنَا إِلَّا نَاضِحَانِ فَحَجَّ أَبُو وَلَدِهَا وَابْنُهَا عَلَى نَاضِحٍ وَتَرَكَ لَنَا نَاضِحًا نَنْضِحُ عَلَيْهِ، قَالَ: «فَإِذَا جَاءَ رَمَضَانُ فَاعْتَمِرِي، فَإِنَّ عُمْرَةً فِيهِ تَعْدِلُ حَجَّةً».
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia mwanamke mmoja miongoni mwa Ansari (Watu wa Madina) ambaye bin Abbas alimtaja kwa jina, lakini mimi nimelisahau jina lake: “Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi?” Akasema: Sisi tulikuwa na vilemba viwili tu, basi baba wa mwanawe na mwanawe walihiji kwa kilemba hicho na akatuachia kilemba kimoja ili tukifue.” Akasema: «Basi itakapokuja Ramadhani, basi fanya Umra, kwani Umra ndani ya Ramadhani ni sawa na Hija.”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, aliporejea kutoka katika Hija ya kuaga, alimwambia mwanamke mmoja wa Ansari ambaye hakuhiji: Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi? Akatoa udhuru kwa sababu walikuwa na ngamia wawili, hivyo mume wake na mwanawe walihiji kwa mmoja wao, na kumwacha mwingine akichota maji kisimani. Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, akamwambia kuwa kufanya Umra katika mwezi wa Ramadhani ni sawa na malipo ya Hija.

Mafunzo
  1. Fadhila za Umra ndani ya mwezi wa Ramadhani.
  2. Umra ndani ya Ramadhani inalingana sawa na Hija katika malipo, haina maana ya kuondosha uwajibu wa Hija.
  3. Malipo ya matendo huzidi kulingana na utukufu wa nyakati, ikiwemo matendo yanayofanywa ndani ya Ramadhani.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 19) (1863). صحيح مسلم (2/ 917) (1256). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 403). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 896). المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، للنووي (9/ 2).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «مَنْ حَجَّ لِلهِ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ رَجَعَ كَيَوْمِ وَلَدَتْهُ أُمُّهُ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye hiji kwa kutaka radhi za Allah Mtukufu na akawa hakufanya yasiyofaa; Na yasiyofaa hapa maana yake ni tendo la ndoa na vitangulizi vyake, kama busu, kugusana, neno hili hutumika pia kumaanisha maneno machafu, na akawa hakufanya uovu; kwa kufanya maasi na madhambi, Na miongoni mwa uovu ni kufanya makatazo ya ihiramu (Hija), atarudi kutoka katika hija yake akiwa kasamehewa, kama azaliwavyo mtoto akiwa amesalimika kutokana na madhambi.

Mafunzo
  1. Uwovu pamoja na kuwa umekatazwa katika hali zote, katazo hilo linatiwa mkazo katika Hija kwa kuheshimu na kutukuza ibada ya Hija.
  2. Mwanadamu huzaliwa pasina kuwa na makosa akiwa kaepukana na madhambi; hivyo hawezi kubeba madhambi ya mwingine.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 133) (1521). صحيح مسلم (2/ 983) (1350). رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين (ص358) (1274). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 401). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (15/ 378). شرح رياض الصالحين، للشيخ محمد بن صالح العثيمين (5/ 321). شرح النووي على مسلم (9/ 119). إكمال المعلم بفوائد مسلم، للقاضي عياض (4/ 462).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنِينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا أَنَّهَا قَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، نَرَى الجِهَادَ أَفْضَلَ العَمَلِ، أَفَلاَ نُجَاهِدُ؟ قَالَ: «لَا، لَكُنَّ أَفْضَلُ الجِهَادِ: حَجٌّ مَبْرُورٌ».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa."
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Maswahaba Mwenyezi Mungu awawie radhi, waliona Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kupigana na maadui kuwa ni matendo bora, Basi Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akamuuliza Mtume Rehema na Amani zimshukie, je nao wapigane Jihadi? Basi rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akawaelekeza kwenye Jihadi bora zaidi kwao, ambayo ni Hija iliyokubalika kwa mujibu wa Qur’ani na Sunna, isiyo na dhambi na unafiki (Riyaa).

Mafunzo
  1. Jihadi ni katika amali bora kwa wanaume.
  2. Haji kwa wanawake ni bora kuliko Jihadi, na ni miongoni mwa matendo bora kwao.
  3. Amali zinazidiana ubora na zinatofautiana kulingana na mfanyaji.
  4. Hija inaitwa Jihad; Kwa sababu ni Jihadi kwa ajili ya nafsi, na inahusisha kutoa mali na nguvu ya mwili, hivyo ni ibada ya mwili na mali kama kupigana Jihadi kwa ajili ya Allah.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 133) (1520). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 402). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 902). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 321).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasikini na madhambi kama moto unavyoondoa uchafu wa chuma, na dhahabu, na fedha, na haina Hija nzuri na safi malipo isipokuwa Pepo

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تَابِعُوا بَيْنَ الحَجِّ وَالعُمْرَةِ، فَإِنَّهُمَا يَنْفِيَانِ الفَقْرَ وَالذُّنُوبَ كَمَا يَنْفِي الكِيرُ خَبَثَ الحَدِيدِ، وَالذَّهَبِ، وَالفِضَّةِ، وَلَيْسَ لِلْحَجَّةِ الْمَبْرُورَةِ ثَوَابٌ إِلاَّ الجَنَّةُ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasikini na madhambi kama moto unavyoondoa uchafu wa chuma, na dhahabu, na fedha, na haina Hija nzuri na safi malipo isipokuwa Pepo".
Imepokelewa naTirmidhiy na Nasai na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka karibu kati ya kutimiza ibada ya Hija na ibada ya Umra, na kutoacha kuzitekeleza hali yakuwa kuna uwezo, kwa sababu kuzitekeleza kwake inakuwa ni sababu ya kuondoa umasikini na madhambi na athari zake ndani ya moyo, kama ambavyo mpulizo wa moto huwa sababu ya kuondoa uchafu wa chuma na vyote vinavyochanganyika nacho katika madini ambayo si chuma.

Mafunzo
  1. Fadhila za kufuatanisha baina ya Hija na umra na himizo katika hilo.
  2. Kufuatanisha kati ya Hija na Umra ni miongoni mwa sababu za utajiri na msamaha wa madhambi.
  3. Amesema Al-Mubaarakafuriy: (Huondoa umasikini) Yaani: Huuondosha kabisa, na hii inategemea maana zote mbili: Umasikini unaoonekana kwa kupatikana utajiri wa mkononi, na umasikini wa ndani, kwa kupata utajiri wa moyo.
Marejeo

سنن الترمذي (2/ 167) (810)، سنن النسائي (5/ 115) (2631)، مسند أحمد (6/ 185) (3669)، ذخيرة العقبى في شرح المجتبى (23/ 322). النهاية في غريب الحديث والأثر (819) (252).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com