Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu siku kumi za mwisho wa Ramadhani, mpaka alimpomfisha Mwenyezi Mungu, kisha wakakaa itikafu wake zake baada yake

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَعْتَكِفُ العَشْرَ الأَوَاخِرَ مِنْ رَمَضَانَ، حَتَّى تَوَفَّاهُ اللَّهُ، ثُمَّ اعْتَكَفَ أَزْوَاجُهُ مِنْ بَعْدِهِ.
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu siku kumi za mwisho wa Ramadhani, mpaka alimpomfisha Mwenyezi Mungu, kisha wakakaa itikafu wake zake baada yake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alidumu na itikafu katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, kwa ajili ya kuutafuta usiku wenye cheo (Lailatul-Qadri), na akaendelea katika hilo mpaka Mwenyezi Mungu alipomfisha, na wakadumu na itikafu wake zake baada yake, radhi za Allah ziwe juu yao.

Mafunzo
  1. Sheria ya kukaa itikafu misikitini, hata kwa wanawake kwa kuzingatia vigezo vya kisheria, na kwa sharti la kuwa na amani dhidi ya fitina.
  2. Inakuwa na mkazo itikafu katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani kwa kudumu nazo Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Itikafu ni sunna endelevu wala haikufutwa, kwani walikaa itikafu wake zake Mtume rehema na amani ziwe juu yake baada yake.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 47) (2026). صحيح مسلم (2/ 831) (1172). تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص351). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 474).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kufanya Itikafu.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com