Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Funga za Kujikurubisha.

Hadithi 3

Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wake na moto miaka sabini

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَنْ صَامَ يَوْمًا فِي سَبِيلِ اللهِ بَاعَدَ اللهُ وَجْهَهُ عَنِ النَّارِ سَبْعِينَ خَرِيفًا».
Imepokelewa na Abii Said Al-khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wake na moto miaka sabini".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayefunga siku moja katika Jihadi na kwingineko kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa kutafuta thawabu na malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu; basi Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake ataweka mbali baina yake na moto miaka sabini.

Mafunzo
  1. Amesema Nawawi: Fadhila za kufunga katika njia ya Mwenyezi Mungu, na hili linachukuliwa kwa yule ambaye hadhuriki kwa swaumu hiyo, na wala hapotezi haki zake, na wala hatopoteza mapambano yake wala kinginecho katika majukumu mapigano yake.
  2. Himizo na hamasisho la kufunga swaumu ya hiyari.
  3. Uwajibu wa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na wala asifunge kwa kujionyesha wala kutaka kusikika, wala kwa makusudio mengine.
  4. Amesema As-sanadi: Kauli yake "Katika njia ya Mwenyezi Mungu", inategemea kuwa masukudio yake ni nia pekee, na inawezekana kuwa makusudio yake nikuwa amefunga akiwa katika hali ya vitani, na la pili ndio liko karibu na usawa.
  5. Amesema bin Hajari: Kauli yake: "Viangazi sabini" Kiangazi ni wakati maalumu wa mwaka, na makusudio yake hapa ni mwaka, na kutajwa kiangazi pekee hapa pasina kutaja wakati uliobakia -kama kiangazi na masika, na kipupwe-; kwa sababu kiangazi ndio kipindi kizuri zaidi kwani hua ndio muda wa kuvuna matunda.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 26) (2840). صحيح مسلم (2/ 808) (1153). تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص346). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 465). الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص426). خلاصة الكلام على عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص162).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu yake kwa mambo matatu: kufunga siku tatu katika kila mwezi, na rakaa mbili baada ya kuchomoza jua (Dhuhaa), na nisali witiri kabla sijalala

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: أَوْصَانِي خَلِيلِي صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِثَلاَثٍ: صِيَامِ ثَلاَثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ، وَرَكْعَتَيِ الضُّحَى، وَأَنْ أُوتِرَ قَبْلَ أَنْ أَنَامَ.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu yake kwa mambo matatu: kufunga siku tatu katika kila mwezi, na rakaa mbili baada ya kuchomoza jua (Dhuhaa), na nisali witiri kabla sijalala".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa kipenzi chake na jamaa yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuusia na akamsisitizia mambo matatu: La kwanza: Kufunga siku tatu katika kila mwezi. La pili: Rakaa mbili za Dhuhaa kila siku. La tatu: Kusali witiri kabla ya kulala; na hii ni kwa mtu atakayehofia kutoamka mwisho wa usiku.

Mafunzo
  1. Kutofautiana kwa usia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Masahaba zake: Hii inasababishwa na elimu yake rehema na amani ziwe juu yake ya kujua hali za Masahaba zake, na kile kinachomfaa kila mmoja miongoni mwao, mwenye nguvu kinachomfaa ni Jihadi, na mchamungu kinachomfaa ni ibada, na mwanachuoni kinachomfaa ni elimu, na kuendelea.
  2. Amesema bin Hajari Al-Asqalaani: Katika kauli yake: Kufunga siku tatu katika kila mwezi, kinachoonekana nikuwa makusudio yake ni masiku meupe, ambayo ni: Siku ya tarehe kumi na tatu, kumi na nne, na kumi na tano, katika kalenda ya Hijiria.
  3. Amesema bin Hajari Al-Asqalani: Hapa inaonyesha kuwa inapendeza kuitanguliza witiri kabla ya kulala, na hii kwa mtu ambaye hana uhakika wa kuamka kuswali.
  4. Umuhimu wa matendo haya matatu; kwa sababu ya usia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwausia idadi kubwa ya Maswahaba zake.
  5. Amesema bin Daqiq Al-Iid katika kauli yake: "Na rakaa mbili za Dhuha": Huenda kataja chache ambazo unapatikana msisitizo wa kuzifanya, na katika hili kuna dalili ya kuwa Dhuha ni sunna, nakuwa kwa uchache ni rakaa mbili.
  6. Wakati wa swala ya Dhuha: Ni baada ya kuchomoza Jua kwa robo saa takriban, na unakwenda wakati wake mpaka kabla ya Adhuhuri kwa dakika kumi takriban, na idadi: Kwa uchache ni rakaa mbili, na zimetofautiana kauli za wanachuoni kuhusu wingi wake; wakasema: Rakaa nane, na wakasema: Hakuna kiwango cha wingi wake.
  7. Wakati wa witiri: Baada ya swala ya Ishaa mpaka kuchomoza Alfajiri, na uchache wake ni rakaa moja, na wingi wake ni rakaa kumi na moja.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 41) (1981). صحيح مسلم (1/ 499) (721). تيسير العلام، للبسام (ص342). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (3/ 456). خلاصة الكلام على عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص159).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima

عَنْ عَبْدَ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّكَ لَتَصُومُ الدَّهْرَ، وَتَقُومُ اللَّيْلَ؟»، فَقُلْتُ: نَعَمْ، قَالَ: «إِنَّكَ إِذَا فَعَلْتَ ذَلِكَ هَجَمَتْ لَهُ العَيْنُ، وَنَفِهَتْ لَهُ النَّفْسُ، لاَ صَامَ مَنْ صَامَ الدَّهْرَ، صَوْمُ ثَلاَثَةِ أَيَّامٍ صَوْمُ الدَّهْرِ كُلِّهِ»، قُلْتُ: فَإِنِّي أُطِيقُ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ، قَالَ: «فَصُمْ صَوْمَ دَاوُدَ عَلَيْهِ السَّلاَمُ، كَانَ يَصُومُ يَوْمًا وَيُفْطِرُ يَوْمًا، وَلاَ يَفِرُّ إِذَا لاَقَى».
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Amru -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika wewe unafunga milele, na unasimama usiku?", Nikasema: Ndiyo, akasema: "Hakika wewe ukifanya hivyo macho yatadhoofu, na nafsi itanyongeka, Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima", Nikasema: Hakika mimi ninaweza zaidi ya hapo, akasema: "Basi funga swaumu Daudi amani iwe juu yake, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja, na wala hakimbii anapokutana (na adui)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ilimfikia habari Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Abdallah bin Amri radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa akiunganisha swaumu na wala hafungui mwaka mzima, na anaswali usiku mzima wala halali, akamkataza hilo na akamwambia: Funga na ufungue, na simama na ulale. Na akamkataza kuunganisha swaumu na kusimama usiku mzima, na akamwambia: Hakika wewe ukifanya hivyo macho yako yatadhoofika na yatabonyea, na itanyong'onyea kwa hilo nafsi yako na itachoka nakuwa na unyonge; hana swaumu atakayefunga mwaka mzima; kiasi ambacho hakupata malipo ya swaumu kwa kwenda kinyume na katazo, na hakufungua kwa sababu aliendelea. Kisha akamuelekeza kufunga siku tatu katika kila mwezi, hizo ni sawa na swaumu ya mwaka mzima; kwa sababu kila siku moja ni sawa na siku kumi, ambayo ndiyo ziada ndogo zaidi ya mema. Akasema Abdullah: Hakika mimi ninaweza zaidi ya hizo. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Basi funga swaumu ya Daudi amani iwe juu yake na ndiyo swaumu bora, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja, na alikuwa hakimbii anapokutana na adui; kwa sababu namna ya swaumu yake haikudhoofisha mwili wake.

Mafunzo
  1. Kufunga siku tatu katika kila mwezi ni kama kufunga mwaka mzima, na hii ni kwa sababu jema moja hulipwa mara kumi mfano wake, zinakuwa siku thelathini, akifunga katika kila mwezi siku tatu anakuwa kana kwamba kafunga mwaka mzima.
  2. Miongoni mwa njia za ufikishaji ujumbe wa Mwenyezi Mungu ni kuhamasisha katika amali na kueleza thawabu zake na thawabu za kudumu na amali hiyo
  3. Amesema Khattwabi: Muhutasari wa kisa cha Abdallah bin Amri nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hajamuwekea ibada ya swaumu pekee mja wake, bali kamuwekea aina mbali mbali za ibada, hata angemaliza juhudi zake zote angepunguza katika ibada zingine, jambo bora ni kuwa kati na kati ili abakishe baadhi ya nguvu kwa ajili ya ibada zingine, na limeashiriwa hilo katika kauli yake rehema na amani ziwe juu yake kwa Daudi amani iwe juu yake: "Na alikuwa hakimbii anapokutana na adui"; kwa sababu alikuwa akipata nguvu kwa kufungua kwa ajili ya Jihadi.
  4. Katazo la kuzama na kujikalifisha katika ibada, na kheri inakuwa kwa kushikamana na sunna.
  5. kauli ya jopo la wanachuoni ni kuchukiza kufunga milele, na inakuwa ni haramu atakapoipa tabu nafsi na akaidhuru, na akaibebesha mzigo mzito, na akaachana na sunna ya Nabii wake rehema na amani ziwe juu yake, na akaitakidi kuwa isiyokuwa sunna yake ndiyo bora kuliko sunna.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 40) (1979). صحيح مسلم (2/ 812) (1159). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 214). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (3/ 297).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com