Nilishuhudia swala ya Idd pamoja na Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Siku mbili hizi alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufunga ndani yake: Siku ya kufungua kwenu kutoka katika swaumu yenu, na siku nyingine ni ile mnayokula katika vichinjwa vyenu
Kutoka kwa Abuu Ubaidi, mwachwa huru wa bin Azhari, amesema: Nilishuhudia swala ya Idd pamoja na Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Siku mbili hizi alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufunga ndani yake: Siku ya kufungua kwenu kutoka katika swaumu yenu, na siku nyingine ni ile mnayokula katika vichinjwa vyenu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufunga siku ya Iddil-Fitiri na Iddil-Adh-ha; ama Iddil-Fitiri ni siku ya kufungua kutoka katika swaumu ya mwezi wa Ramadhani, na ama Iddil-Adh-ha ni siku ya kula katika vichinjwa.
Mafunzo
Uharamu wa kufunga siku mbili za Iddil-Fitiri na Iddil-Adh-ha, na siku tatu za kubanika nyama; kwa sababu zinafuatana na siku ya Iddil-Adh-ha isipokuwa kwa yule ambaye hakupata cha kutoa, itafaa kwake kufunga siku za kubanika nyama.
Amesema bin Hajari: Imesemekana kuwa: Na faida ya kuzitaja siku mbili ni ishara ya kuonyesha sababu ya uwajibu wa kufungua ndani yake, nazo ndio mapumziko ya swaumu, na kudhihirisha ukamilifu wake peke yake kwa kufungua siku zilizo baada yake, na Idd nyingine ni kwa ajili ya kuchinja kwa mwenye kujikurubisha kwa kichinjwa chake ili ale kutoka katika kichinjwa hicho.
Inapendeza kwa mtoa hotuba ataje katika hotuba yake yale yanayohusiana na wakati wake miongoni mwa hukumu, na atumie fursa ya matukio kama hayo.
Sheria ya kula kutoka katika kichinjwa cha ibada.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 42) (1990).
صحيح مسلم (2/ 799) (1137).
تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص344).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 461).
الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص426).
خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص161).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com