Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kufunga siku ya Shaka.

Hadithi 1

Msiitangulizie Ramadhani kwa swaumu ya siku moja wala siku mbili, isipokuwa mtu aliyekuwa akifunga swaumu fulani basi na aifunge

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تَقَدَّمُوا رَمَضَانَ بِصَوْمِ يَوْمٍ وَلَا يَوْمَيْنِ إِلَّا رَجُلٌ كَانَ يَصُومُ صَوْمًا فَلْيَصُمْهُ».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msiitangulizie Ramadhani kwa swaumu ya siku moja wala siku mbili, isipokuwa mtu aliyekuwa akifunga swaumu fulani basi na aifunge".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kufunga kabla ya Ramadhani kwa siku moja au siku mbili, kwa nia ya kuchukua tahadhari kuwa huenda Ramadhani imeingia; kwa sababu ulazima wa Ramadhani umewekwa katika kuonekana kwa mwandamo, na wala hakuna haja ya kujikalifisha, isipokuwa kama mtu alikuwa akifunga swaumu aliyoizoea, kama kufunga siku moja na kula siku moja, au siku ya juma tatu na Alhamisi ikaangukia siku hiyo basi na afunge; na wala hilo halihesabiki kuwa ni katika kuipokea Ramadhani, na inaunganishwa hapo swaumu zitakazokuwa za wajibu kama kulipa deni na swaumu ya nadhiri.

Mafunzo
  1. Katazo la kujilazimisha, na uwajibu wa kuzihifadhi ibada kama zilivyowekwa na sheria pasina kuzidisha au kupunguza.
  2. Miongoni mwa hekima za hilo -na Allah ndiye mjuzi zaidi- ni kutofautisha kati ya ibada za faradhi na sunna, na kujiandaa kwa Ramadhani kwa uchangamfu na shauku, na ili swaumu iwe ndiyo nembo ya mwezi mtukufu yenye kujipambanua nayo.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 28) (1914). صحيح مسلم (2/ 762) (1082). تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص313). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 412).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com