Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Fanyeni haraka kulipeleka jeneza, likiwa ni la mtu mwema, basi mnaliwahisha kupata kheri, na likiwa kinyume na hivyo, basi hiyo nishari mnajiwekea shingoni kwenu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أَسْرِعُوا بِالْجِنَازَةِ، فَإِنْ تَكُ صَالِحَةً فَخَيْرٌ تُقَدِّمُونَهَا، وَإِنْ يَكُ سِوَى ذَلِكَ، فَشَرٌّ تَضَعُونَهُ عَنْ رِقَابِكُمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Fanyeni haraka kulipeleka jeneza, likiwa ni la mtu mwema, basi mnaliwahisha kupata kheri, na likiwa kinyume na hivyo, basi hiyo nishari mnajiwekea shingoni kwenu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwenda mbio kuliandaa jeneza na kuliswalia na kuzika; jeneza likiwa jema basi mnaliwahisha kwenda katika kheri miongoni mwa neema za kaburi, na likiwa kinyuume na hivyo, basi hiyo ni shari mnaiweka katika shingo zenu.

Mafunzo
  1. Amesema bin Hajari: Inapendeza na ni sunna kwenda haraka, lakini kwa kiwango ambacho si cha nguvu, kiasi ambacho yanaweza kuhofiwa madhara kwa maiti, au uzito kwa mbebaji au msindikizaji.
  2. Hapa kuna mpaka katika uharaka, ni pale ikiwa kifo kitakuwa cha ghafla, kwani inahofiwa inaweza kuwa ni kuzimia tu, hapa ni inatakiwa asizikwe ila baada ya kuthibitsha kifo chake, au inaweza kuwa kuchelewesha kidogo kwa ni kwa sababu ya masilahi, kama kuongezeka wa kumswalia, au kuhudhuria ndugu zake wa karibu, endapo hatohofiwa kuharibika.
  3. Himizo la kulipeleka haraka jeneza ni kwa ajili ya masilahi ya maiti akiwa ni mtu mwema, au kwa ajili ya masilahi ya wasindikizaji akiwa ni mtu muovu.
  4. Amesema Nawawi: Na inachukuliwa faida hapa kuwa mtu aache kusuhubiana na watu waovu wasiokuwa wema.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 86) (1315). صحيح مسلم (2/ 651) (944). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص284). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 367).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kumbeba maiti na kumzika.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com