Swali ukiwa umesimama, usipoweza basi swali ukiwa umekaa, usipoweza basi ukiwa umelala ubavu
عن عمران بن حصين رضي الله عنه قال: كَانَتْ بِي بَوَاسِيرُ، فَسَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الصَّلَاةِ، فَقَالَ: «صَلِّ قَائِمًا، فَإِنْ لَمْ تَسْتَطِعْ فَقَاعِدًا، فَإِنْ لَمْ تَسْتَطِعْ فَعَلَى جَنْبٍ».
Kutoka kwa Imran bin Huswain -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Niliugua bawasiri, nikamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kusali, akasema: "Swali ukiwa umesimama, usipoweza basi swali ukiwa umekaa, usipoweza basi ukiwa umelala ubavu".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa asili katika swala ni kusali kwa kusimama, isipokuwa katika hali ya kutoweza hapo mtu atasali kwa kukaa, na ikiwa hatoweza kukaa atasali kwa ubavu.
Mafunzo
- Swala haidondoki kwa muda ambao akili bado ipo, itakuwa kwa kuhama kutoka hali moja kwenda nyingine kadiri ya uwezo.
- Huruma na wepesi wa Uislamu kwa kumpa uhuru mja afanye kadiri awezavyo katika ibada.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 48) (1117). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبدالله البسام (2/ 322). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (3/ 202).