Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hukumu ya Imamu na Maamuma.

Hadithi 6

Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «سَوُّوا صُفُوفَكُمْ، فَإِنَّ تَسْوِيَةَ الصَّفِّ مِنْ تَمَامِ الصَّلَاةِ».
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wenye kuswali kunyoosha safu zao, na wasitanguliane wala wasirudi nyuma, na kwamba kuzinyoosha ni sehemu ya kukamilisha na ukamilifu wa Sala, na kuwa kupinda kwa safu ni dosari na ni upungufu ndani yake.

Mafunzo
  1. Sheria ya kuchunga kila kinachokamilisha swala na kuiweka mbali na upungufu.
  2. Hekima ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kufundisha, kwani aliihusisha hukumu na sababu yake; ili iwe wazi hekima ya kuletwa sheria hiyo, na nafsi ipate hamasa ya kuitekeleza.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 145) (723). صحيح مسلم (1/ 324) (433). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص127). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 161). الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص173).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hivi haogopi mmoja wenu (Au: Hachelei mmoja wenu) atakapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu akifanye kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye Mwenyezi Mungu sura yake kuwa sura ya punda

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أَمَا يَخْشَى أَحَدُكُمْ - أَوْ: لاَ يَخْشَى أَحَدُكُمْ - إِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ قَبْلَ الإِمَامِ، أَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ رَأْسَهُ رَأْسَ حِمَارٍ، أَوْ يَجْعَلَ اللَّهُ صُورَتَهُ صُورَةَ حِمَارٍ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi haogopi mmoja wenu (Au: Hachelei mmoja wenu) atakapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu akifanye kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye Mwenyezi Mungu sura yake kuwa sura ya punda".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kunyanyua kichwa chake kabla ya imamu wake, kuwa Mwenyezi Mungu kukifanya kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye sura yake kuwa sura ya punda.

Mafunzo
  1. Maamuma anapokuwa na imam kuna hali nne: haliTatu zimekatazwa, nazo ni: Kumtangulia, na kwenda naye sawa, na kuchelewa, na mafundisho kwa maamuma: Ni kumfuata imam.
  2. Ulazima wa maamuma kumfuata imam ndani ya swala.
  3. Ahadi ya adhabu ya kubadilika sura kwa atakayenyanyua kichwa chake kabla ya imam na kuwa sura ya punda ni jambo linawezekana, nako ni kufutwa kwa sura halisi.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 140) (691). صحيح مسلم (1/ 321) (427). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 111). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص65). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص133).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema: Sami'allaahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi) alikuwa hanyanyui yeyote miongoni mwetu mgongo wake mpaka aporomoke Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusujudu, kisha nasi tunaporomoka baada yake

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يَزِيدَ الخَطْمِيِّ قَالَ: حَدَّثَنِي البَرَاءُ وَهُوَ غَيْرُ كَذُوبٍ، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَالَ: سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، لَمْ يَحْنِ أَحَدٌ مِنَّا ظَهْرَهُ حَتَّى يَقَعَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَاجِدًا، ثُمَّ نَقَعُ سُجُودًا بَعْدَهُ.
Kutoka kwa Abdallah bin Yazidi Al-Khatmiy amesema: Alinisimulia Al-Baraa naye si mtu wa kukadhibishwa, akasema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema: Sami'allaahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi) alikuwa hanyanyui yeyote miongoni mwetu mgongo wake mpaka aporomoke Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusujudu, kisha nasi tunaporomoka baada yake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Baraa bin Azibi radhi za Allah ziwe juu yake naye ni mkweli, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anasema: Sami'allahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi), walikuwa wakiendelea kusimama walioko nyuma yake, na hainamishi yeyote miongoni mwao mgongo wake kwa ajili ya kusujudu mpaka aweke rehema na amani ziwe juu yake paji lake la uso katika Ardhi, kisha wanaporomoka wote kwa kusujudu baada yake.

Mafunzo
  1. Namna Maswahaba walivyomfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika swala, nakwamba wao walikuwa hawahami kutoka waliposimama kwenda katika sijida mpaka asujudu.
  2. Amesema Bin Daqiiq Al-Idd: Katika hilo kuna ushahidi wa utulivu wa muda mrefu kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Maamuma kwa imamu wake ana hali nne katika kumfuata: 1- Kumtangulia: Kwa kuanza kitendo kabla ya imamu wake, kwa kufika maamuma katika rukuu kabla ya imamu hajafika, mfano: Kama akirukuu kabla ya imamu, au akasujudu kabla ya imamu, na hii ni haramu, na akikusudia kumtangulia huku akijua kuwa imekatazwa kufanya hivyo basi swala yake inaharibika, sawa awe kamtangulia kutoka katika nguzo au kwenda katika nguzo, na ikiwa ni katika takbira ya kuanza swala (ile ya kuhirimia swala) basi swala yake haitokubalika, na itamlazimu arudie upya swala yake. 2- Kwenda naye sawa, aende sawa na imamu, arukuu pamoja na rukuu yake na asujudu na sijida yake, na anyanyuke pamoja na kunyanyuka kwake, na kitendo hiki kwa uchache kabisa ni machukizo, na uwazi wa dalili unaonyesha kuwa ni haramu pia; na akienda sawa na imamu katika takbira ya kuanza swala, swala yake haitokubalika na atalazimika kurudia swala yake. 3- Kumfuata: Kwa kuleta vitendo vya swala baada ya imamu wake, pasina kuchelewa, na hii ndio namna bora na ya kisheria. 4- Kwenda kinyume naye, kwa kwenda kinyume na imamu wake kiasi ambacho kinamtoa katika kumfuata, kama imamu kurukuu na akabakia maamuma kasimama mpaka imamu akakaribia kunyanyuka kutoka katika rukuu, na hii ni kinyume na sheria na ni haramu, isipokuwa ikiwa ni kwa sababu ya maradhi au utu uzima.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 140) (690). صحيح مسلم (1/ 345) (474). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 114). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص139).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake

عَنْ وَابِصَةَ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَأَى رَجُلًا صَلَّى وَحْدَهُ خَلْفَ الصَّفِّ، فَأَمَرَهُ أَنْ يُعِيدَ صَلَاتَهُ.
Kutoka kwa Waabiswa radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja aliyeswali nyuma ya safu peke yake, akamuamrisha arudie swala yake; kwa sababu swala yake haikusihi kwa hali hii.

Mafunzo
  1. Himizo la kuwahi swala ya jamaa na kuwahi mbele kwa ajili yake, na asiswali nyuma ya safu peke yake ili swala yake asiitie katika kubatilika
  2. Amesema bin Hajari: Atakayeanza swala peke yake nyuma ya safu kisha akaingia katika safu kabla ya kunyanyuka kutoka katika rukuu, hatolazimika kurudia, kama ilivyokuja katika hadithi ya Abiibakra, na vinginevyo itakuwa wajibu kwa mujibu wa ujumla wa hadithi ya Waabiswa.
Marejeo

سنن أبي داود (2/ 18) (682). سنن الترمذي (1/ 268) (230). سنن ابن ماجه (2/ 137) (1004). مسند أحمد (29/ 524) (18000). سبل السلام شرح بلوغ المرام، لمحمد الصنعاني (1/ 378). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 509). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (2/ 288).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, basi na afanye kama anavyofanya

عن علي بن أبي طالب، ومعاذ بن جبل رضي الله عنهما مرفوعًا: «إذا أتى أحدُكم الصلاةَ والإمامُ على حال، فلْيصنعْ كما يصنع الإمامُ».
Kutoka kwa Ally bin Abii Twalib, na Mua'dh bin Jabali- radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, basi na afanye kama anavyofanya imamu".
Imepokelewa na Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, ima ya kusimama au kurukuu au kusujudu au kukaa, basi aendane na imamu pale alipo katika kusimama au kurukuu au kitendo kinginecho, na asisubiri mpaka anyanyuke imamu kama wanavyofanya baadhi ya watu.

Mafunzo
  1. Sheria ya kuingia mwenye kuungana pamoja na imamu katika kipengele chochote miongoni mwa vipengele vya swala atakachokikuta, bila kutofautisha kati ya rukuu na sijida na kukaa.
  2. Nikuwa kuipata rakaa ambayo ameungana na imamu kunakuwa kwa kuikuta rukuu yake, kama zilivyoonyesha juu ya hilo dalili zingine.
Marejeo

سنن الترمذي، محمد بن عيسى الترمذي، تحقيق وتعليق: أحمد محمد شاكر، ومحمد فؤاد عبد الباقي، وإبراهيم عطوة عوض، شركة مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي، مصر، الطبعة الثانية، 1395هـ - 1975م. نيل الأوطار، محمد بن علي الشوكاني اليمني، تحقيق: عصام الدين الصبابطي، الناشر: دار الحديث، مصر، الطبعة الأولى، 1413هـ - 1993م. صحيح الجامع الصغير وزيادته، محمد ناصر الدين الألباني، المكتب الإسلامي، بيروت، الطبعة الثالثة، 1408هـ. تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، محمد عبد الرحمن بن عبد الرحيم المباركفورى، دار الكتب العلمية، بيروت. بلوغ المرام من أدلة الأحكام، أحمد بن علي بن حجر العسقلاني، دار القبس للنشر والتوزيع، الرياض، المملكة العربية السعودية، الطبعة الأولى، 1435هـ - 2014م.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Pindi mtakaposwali basi nyoosheni safu zenu, kisha akuongozeni mmoja wenu, atakapotoa takbira basi toeni takbira

عَنْ ‌حِطَّانَ بْنِ عَبْدِ اللهِ الرَّقَاشِيِّ قَالَ: صَلَّيْتُ مَعَ ‌أَبِي مُوسَى الْأَشْعَرِيِّ صَلَاةً، فَلَمَّا كَانَ عِنْدَ الْقَعْدَةِ قَالَ رَجُلٌ مِنَ الْقَوْمِ: أُقِرَّتِ الصَّلَاةُ بِالْبِرِّ وَالزَّكَاةِ، قَالَ: فَلَمَّا قَضَى أَبُو مُوسَى الصَّلَاةَ وَسَلَّمَ انْصَرَفَ فَقَالَ: أَيُّكُمُ الْقَائِلُ كَلِمَةَ كَذَا وَكَذَا؟ قَالَ: فَأَرَمَّ الْقَوْمُ، ثُمَّ قَالَ: أَيُّكُمُ الْقَائِلُ كَلِمَةَ كَذَا وَكَذَا؟ فَأَرَمَّ الْقَوْمُ، فَقَالَ: لَعَلَّكَ يَا حِطَّانُ قُلْتَهَا؟ قَالَ: مَا قُلْتُهَا، وَلَقَدْ رَهِبْتُ أَنْ تَبْكَعَنِي بِهَا، فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الْقَوْمِ: أَنَا قُلْتُهَا، وَلَمْ أُرِدْ بِهَا إِلَّا الْخَيْرَ، فَقَالَ أَبُو مُوسَى: أَمَا تَعْلَمُونَ كَيْفَ تَقُولُونَ فِي صَلَاتِكُمْ؟ إِنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَطَبَنَا فَبَيَّنَ لَنَا سُنَّتَنَا وَعَلَّمَنَا صَلَاتَنَا، فَقَالَ: «إِذَا صَلَّيْتُمْ فَأَقِيمُوا صُفُوفَكُمْ، ثُمَّ لِيَؤُمَّكُمْ أَحَدُكُمْ فَإِذَا كَبَّرَ فَكَبِّرُوا، وَإِذْ قَالَ: {غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلا الضَّالِّينَ} [الفاتحة: 7]، فَقُولُوا: آمِينَ، يُجِبْكُمُ اللهُ، فَإِذَا كَبَّرَ وَرَكَعَ فَكَبِّرُوا وَارْكَعُوا، فَإِنَّ الْإِمَامَ يَرْكَعُ قَبْلَكُمْ، وَيَرْفَعُ قَبْلَكُمْ»، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «فَتِلْكَ بِتِلْكَ، وَإِذَا قَالَ: سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، فَقُولُوا: اللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ الْحَمْدُ، يَسْمَعِ اللهُ لَكُمْ، فَإِنَّ اللهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى قَالَ عَلَى لِسَانِ نَبِيِّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، وَإِذَا كَبَّرَ وَسَجَدَ فَكَبِّرُوا وَاسْجُدُوا، فَإِنَّ الْإِمَامَ يَسْجُدُ قَبْلَكُمْ وَيَرْفَعُ قَبْلَكُمْ»، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «فَتِلْكَ بِتِلْكَ، وَإِذَا كَانَ عِنْدَ الْقَعْدَةِ فَلْيَكُنْ مِنْ أَوَّلِ قَوْلِ أَحَدِكُمُ: التَّحِيَّاتُ الطَّيِّبَاتُ الصَّلَوَاتُ لِلهِ، السَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا النَّبِيُّ وَرَحْمَةُ اللهِ وَبَرَكَاتُهُ، السَّلَامُ عَلَيْنَا وَعَلَى عِبَادِ اللهِ الصَّالِحِينَ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ».
Kutoka kwa Hittwan bin Abdillah Ar-Raqashi amesema: Nilisali pamoja na Abuu Mussa Al-Ash'ariy swala moja, tulipofika katika kikao (cha tahiyatu) mtu mmoja akasema: Swala imefungamanishwa na wema na zaka, akasema: Abuu Mussa alipomaliza swala na akatoa salamu, akageuka na akasema: Ni nani kati yenu aliyesema neno kadhaa wa kadhaa? Akasema: Watu wote wakanyamaza, kisha akasema: Ni nani kati yenu aliyesema neno kadhaa wa kadhaa? Watu wote wakanyamaza, akasema: Huenda ukawa ni wewe uliyesema ewe Hittwan? Akasema: Hakika niliogopa utaninyamazisha kwa neno hilo, akasema mtu mmoja katika jamaa waliokuwepo: Mimi ndiye niliyesema, na sikukusudia kwa neno hilo ila kheri, Abuu Mussa akasema: Hivi hamjui ni vipi mtasema ndani ya swala zenu? hakika Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alituhutubia na akatubainishia sunna zetu na akatufundisha swala yetu, akasema: "Pindi mtakaposwali basi nyoosheni safu zenu, kisha akuongozeni mmoja wenu, atakapotoa takbira basi toeni takbira, na anaposema: "Ghairil maghdhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" [Suratul Fatiha: 7], basi semeni: Aaamiin (Ewe Mola wetu Mlezi tukubalie maombi) Atakujibuni Mwenyezi Mungu, atakapotoa takbira na akarukuu basi nanyi toeni takbira na mrukuu, kwani imamu anatakiwa kurukuu kabla yenu, na anyanyuke kabla yenu", akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:"Hiyo itakwenda na ile, na akisema: Samia'llaahu liman hamidah, semeni: Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, Mwenyezi Mungu anakusikieni, kwani Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- alisema kupitia ulimi wa Nabii wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi, na akitoa takbira akasujudu basi sujuduni, kwani imamu anatakiwa asujudu kabla yenu na anyanyuke kabla yenu", akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hiyo inakwenda ile, na akifika mahali pa kukaa basi kauli ya mwanzo ya mmoja wenu iwe ni: Attahiyyatut twayyibaatu as swalawaatu lillaah, assalaam alaika ayyuhan nabiyyu warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu alainaa wa alaa ibaadillaahis swaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu wa ash-hadu anna Muhammadan abduhu warasuuluhu".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Swahaba Abuu Mussa Al-Ash'ary -Radhi za Allah ziwe juu yake- alisali swala moja, alipofika katika kikao cha tahiyatu ambacho kinatashahudi, mtu mmoja akasema miongoni mwa wasaliji walioko nyuma yake: Swala imeunganishwa ndani ya Qur'ani na wema na zaka, Abuu Mussa -Radhi za Allah ziwe juu yake- alipomaliza swala aliwageukia maamuma, akawauliza: Ni nani kati yenu aliyesema neno: Swala imeunganishwa ndani ya Qur'ani na wema na zaka?!, Watu wote wakanyamaza, na hakuzungumza yeyote kati yao, akarudia kuwauliza swali mara nyingine, alipoona hakuna alliyemjibu, Abuu Mussa -Radhi za Allah ziwe juu yake- akasema: Huenda ukawa ni wewe Hittwan ndiye uliyesema! Kwa ujasiri wake na ukaribu wake kwake, na mahusiano yake kwake, jambo ambalo haliwezi kupelekea kumtuhumu, na ili ampe msukumo msemaji wa uhakika kukiri, Hittwan akalikanusha hilo, na akasema, nilihofia unaweza kunikaripia kwa kudhani kuwa mimi ndiye niliyesema; na hapa sasa yule bwana akazungumza: Mimi ndiye niliyesema, na sikukusudia ila jambo la kheri, Abuu Mussa akasema kwa kumfundisha: Hivi hamjui ni nini mtasema ndani ya swala yenu?! Alisema hivi kwa kukemea kitendo hicho, kisha Abuu Mussa akaeleza kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwahutubia siku moja, akawabainishia sheria zao, na akawafundisha swala yao, akasema -Rehema na amani ziwe juu yake-: Mtakaposali basi nyoosheni safu zenu, na mlingane sawa, kisha mmoja miongoni mwao awasalishe watu, imamu atakapotoa takbira ya kuhirimia swala, basi toeni takbira mfano wake, na akisoma suratul Fatiha na akafikia: "Ghairil magh-dhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" [Fatiha: 7], Semeni: Aaamiin; mkifanya hivyo Mwenyezi Mungu atakujibuni maombi yenu, akitoa takbira na akarukuu basi toeni takbira na mrukuu; kwani imamu anarukuu kabla yenu na ananyanyuka kabla yenu msimtangulie; kwa sababu mahali alipowatangulia imamu ni katika kuwatangulia kurukuu, kutamalizika kwa kuchelewa kwenu kidogo baada ya yeye kunyanyuka kidogo, kitambo hicho kidogo kitapishana kidogo na kunyanyuka kwake, na hapo kiwango cha rukuu yenu kitakuwa sawa na rukuu yake, na imamu akisema: Samiallaahu liman hamidah, basi semeni: Allaahumma Rabbanaa walakal hamdu, waswaliji wakisema hivyo basi hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anasikia dua zao na kauli zao, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema kwa ulimi wa Nabii -Rehema na amani ziwe juu yake-:Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumuhimidi, kisha imamu akitoa takbira na kusujudu basi na maamuma wanatakiwa kutoa takbira na kusujudu, kwani imamu anatakiwa asujudu kabla yao, na anyanyuke kabla yao, kiwango hicho kidogo cha kusubiri kitakuwa sawa na kiwango chake, na hapo kiwango cha maamuma kitakuwa sawa na kiwango cha imamu, ana akifika katika kikao cha tahiyatu, na iwe kauli ya mwanzo ya mwenye kusali ni: "Attahiyyatut twayyibaatu asswalawaatu lillaah" Ufalme na kubakia na utukufu wote unamstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, na vile vile swala tano zote ni za Mwenyezi Mungu, "Assalaamu alaika ayyuhan nabiyyu warahmatullaahi wabarakaatuh", "Assalaamu alainaa walaa ibaadillaahis swaalihiin, muombe Mwenyezi Mungu akusalimishe na kila aibu na maafa, na mapungufu na maovu; na tunamtaja Muhammadi pekee kwa kumtakia amani, kisha tunajitakia amani wenyewe, kisha tunawatakia amani waja wema wa Mwenyezi Mungu wale wenye kutekeleza haki zilizo juu yao za Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za waja wake, kisha tunashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na tunashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na Mtume wake.

Mafunzo
  1. kumebainishwa namna miongoni mwa aina za tashahudi.
  2. Maneno ya swala na vitendo vyake lazima yawe yamethibiti kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, haruhusiwi yeyote kuzua ndani ya swala kuli au kitendo ambacho hakikuthibiti ndani ya sunna.
  3. Haitakiwi kumtangulia imamu au kuchelewa kumfuata, na sheria kwa maamuma ni kumfuata imamu katika vitendo vyake.
  4. Kumetajwa yale aliyokuwa akiyafanya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ikiwemo kutilia umuhimu kufikisha ujumbe, na kuufundisha umma wake hukumu za dini.
  5. Imamu ndio kiigizo kwa maamuma, hatakiwi kumtangulia katika matendo ya swala na wala asiende nae sawa, na wala asichelewe kumfuata, bali kumfuata kwake kuanzie baada ya kuhakikisha kuwa kaingia katika kitendo anachotaka kukifanya, na sunna ni kumfuata.
  6. Sheria ya kunyoosha safu katika swala.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 303) (404)، إكمال المعلم (2/298)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (2/ 37)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص376) (87)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (9/ 402).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com