Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni swala kwa wakati wake", Akasema: Kisha ipi? Akasema: "Kisha wema kwa wazazi wawili" Akasema: "Kisha ipi? "Akasema: "Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu" Akasema: Alinihadithia mambo hayo, na lau ningemtaka ziada angenizidishia.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Aliulizwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu?. Akasema: Ni swala za faradhi katika wakati wake uliopangwa na sheria, Kisha wema kwa wazazi wawili, kwa kuwafanyia wema, na kusimamia haki zao, na kuacha kuwaasi, kisha Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuitetea dini ya Uislamu na waislamu, na kudhihirisha alama zake, na hii inakuwa kwa nafsi na mali.
Akasema bin Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake: Alinieleza amali hizi; na lau kama ningelimwambia: Kisha ipi? Basi angenizidishia.
Mafunzo
Kuzidiana kwa amali kati yake ni kulingana na mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa amali hiyo.
Himizo kwa muislamu katika kupupia amali bora kisha inayofuata kwa ubora.
Kutofautiana kwa majibu ya Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuhusu amali bora kulingana na watu na hali zao, na kulingana na lenye manufaa mengi kwa kila mmoja miongoni mwao.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 112) (527).
صحيح مسلم (1/ 90) (85).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 70).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص84).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 108).
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إِنَّ أَثْقَلَ صَلَاةٍ عَلَى الْمُنَافِقِينَ صَلَاةُ الْعِشَاءِ وَصَلَاةُ الْفَجْرِ، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِيهِمَا لَأَتَوْهُمَا وَلَوْ حَبْوًا، وَلَقَدْ هَمَمْتُ أَنْ آمُرَ بِالصَّلَاةِ فَتُقَامَ، ثُمَّ آمُرَ رَجُلًا فَيُصَلِّيَ بِالنَّاسِ، ثُمَّ أَنْطَلِقَ مَعِي بِرِجَالٍ مَعَهُمْ حُزَمٌ مِنْ حَطَبٍ إِلَى قَوْمٍ لَا يَشْهَدُونَ الصَّلَاةَ، فَأُحَرِّقَ عَلَيْهِمْ بُيُوتَهُمْ بِالنَّارِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika swala nzito zaidi kwa wanafiki ni swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, na lau kama wangejua (malipo) yaliyomo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa, na nilipania niamrishe swala ikimiwe(kusimamishwa), kisha nimuamrishe mtu mmoja awasalishe watu, kisha niondoke pamoja na wanaume wakiwa wamebeba mizigo ya kuni tuelekee kwa watu ambao hawahudhurii swala, ili niwachome na moto wakiwa ndani ya majumba yao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu wanafiki na uvivu wao wa kuhudhuria swala, hasa hasa swala mbili, Ishaa na Alfajiri, nakuwa laiti wangelijua kiwango cha malipo na thawabu katika kuzihudhuria swala hizo pamoja na jamaa ya waislamu, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa mfano wa kutambaa kwa mtoto kwa mikono na magoti.
Bila shaka aliazimia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aamrishe swala ikimiweisimamishwe), na amuweke mtu awasalishe watu badala yake, kisha aondoke akiwa pamoja na watu watakaombebea mizigo ya kuni kwenda kwa watu wasiohudhuria swala ya pamoja (Jamaa) ili awachome wakiwa ndani ya majumba yao; kwa sababu ya ubaya wa waliyoyafanya katika madhambi, -lakini hakufanya hivyo- kwa sababu ndani ya majumba yao kuna wanawake na watoto wasio na hatia, na wengineo miongoni mwa wenye udhuru, wasiokuwa na dhambi.
Mafunzo
Hatari ya kuchelewa swala ya pamoja msikitini.
Wanafiki hawakukusudia katika ibada zao isipokuwa kujionyesha na kutaka kusikika, hawaji katika swala ila katika wakati ambao watu wanawaona.
Malipo makubwa katika swala mbili, Ishaa na Alfajiri kwa jamaa, nakuwa swala hizo zinastahiki zaidi kuziendea hata kwa kutambaa.
Kuhifadhi swala mbili, Ishaa na Alfajiri ni sababu ya kusalimika na unafiki, na kuto kuzihudhuria ni katika sifa za wanafiki.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 451) (651).
صحيح البخاري (1/ 132) (657).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 88).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص107).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 136).
Imepokelewa kutoka kwa Jariri Bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimpa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kusikia na kutii, na nasaha kwa kila muislamu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza swahaba Jariiri Bin Abdallah radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye alishikamana na maamrisho na akampa ahadi Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kutekeleza swala tano za faradhi usiku na mchana, kwa kutimiza sharti zake na nguzo zake na wajibu zake na sunna zake, na kutelekeza zaka ya wajibu, nayo ni ibada ya mali ya lazima, huchukuliwa toka kwa matajiri na kupewa wanaostahiki katika mafakiri na wengineo, na kuwatii viongozi, na kumpa nasaha kila muislamu, na hii ni kwa kuchunga masilahi yake, na kumfikishia kheri, na kumkinga na shari kwa kauli na vitendo.
Mafunzo
Umuhimu wa swala na zaka, nazo ni katika nguzo za Uislamu.
Umuhimu wa nasaha na kunasihiana kati ya waislamu, mpaka wakampa ahadi ya utiifu Masahaba radhi za Allah ziwe juu yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 111) (524)، (3/ 72) (2157).
صحيح مسلم (1/ 75) (56).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 272).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص145).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 398).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 206).
وعن جابر رضي الله عنه قال: سُئِل رسول الله صلى الله عليه وسلم أي الصلاة أفضل؟ قال: «طُول القُنُوتِ».
Na kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Aliulizwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: Ni swala ipi bora? Akasema: "Ni kurefusha kisimamo".
Imepokelewa na Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Walimuuliza maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- : Ni swala ipi bora? Na swali hili ni kwasababu ya pupa yao ya kuhakikisha wanapata kiwango kikubwa cha mema,Na makusudio yake:Ni aina ipi ya swala zote ndio bora? Au: Yaani ni tendo lipi katika matendo ya swala ndio bora? Ni kusimama au kurukuu au kusujudu? Akaeleza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuwa ni kurefusha kisimamo ndani yake.
Marejeo
رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين؛ للإمام أبي زكريا النووي، تحقيق د. ماهر الفحل، دار ابن كثير-دمشق، الطبعة الأولى، 1428ه .
- نزهة المتقين شرح رياض الصالحين؛ تأليف د. مصطفى الخِن وغيره، مؤسسة الرسالة-بيروت، الطبعة الرابعة عشر، 1407هـ.
- صحيح مسلم؛ للإمام مسلم بن الحجاج، حققه ورقمه محمد فؤاد عبد الباقي، دار عالم الكتب-الرياض، الطبعة الأولى، 1417هـ.
- تطريز رياض الصالحين؛ تأليف فيصل آل مبارك، تحقيق د. عبد العزيز آل حمد، دار العاصمة-الرياض، الطبعة الأولى، 1423هـ.
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يقول: «الصَّلَوَاتُ الْخَمْسُ، وَالْجُمُعَةُ إِلَى الْجُمُعَةِ، وَرَمَضَانُ إِلَى رَمَضَانَ، مُكَفِّرَاتٌ مَا بَيْنَهُنَّ إِذَا اجْتَنَبَ الْكَبَائِرَ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema: "Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa swala tano za faradhi za usiku na mchana, na swala ya ijumaa kila wiki, na funga ya Ramadhani kila mwaka, vyote hivi hufuta madhambi madogo madogo yaliyo kati yake, kwa sharti la kuyaepuka madhambi makubwa, Ama madhambi makubwa kama zinaa na kunywa pombe haya hayafutwi isipokuwa kwa toba.
Mafunzo
Madhambi yako madogo madogo na yako makubwa.
Kufutiwa madhambi madogo madogo kumewekwa sharti la ya kuyaepuka makubwa.
Madhambi makubwa ni yale iliyokuja adhabu ndani yake katika dunia, au yaliyotajwa kuwa na ahadi ya adhabu huko Akhera; au Makasiriko, au kukawa na kemeo ndani yake, au kulaaniwa mfanyaji wake, kama zinaa na unywaji pombe.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 209) (233).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 183).
نزهة المتقين بشرح رياض الصالحين، لمصطفى سعيد الخن (1/ 158).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص108).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم بن عيد الهلالي (1/ 209).
Kutoka kwa Ma'adan Bin Abi Twalha Alya'mary amesema: Nilikutana na Thauban muachwa huru wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikasema: 'Niambie matendo nitakayo yafanya (iwe sababu kwa Allah) kuniingiza Peponi' au alisema, nikasema: matendo mazuri yanayopendeka zaidi kwa Allah, akanyamaza, kisha nikamuuliza akanyamaza, kisha nikamuuliza kwa mara ya tatu akasema: Nilimuuliza hayo Mtume wa Allah rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Shikamana na kusujudu kwa wingi kwa ajili ya Allah, kwani hakika wewe huta sujudu kwa ajili ya Allah isipokuwa Allah atakupandisha kwa sijida hiyo daraja, na atakufutia kwa sijida hiyo makosa" Akasema Maadan: Kisha nikakutana na Abuudardaa nikamuuliza, akanambia mfano wa hayo alionambia Thauban.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu matendo yanayopelekea kuingia Peponi au kuhusu matendo yanayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu?
Basi rehema na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia muulizaji: Dumu na sijida kwa wingi, kwani kila unapomsujudia Mwenyezi Mungu anakunyanyua daraja kwayo, na anakusamehe dhambi kwa sababu ya sijida hiyo.
Mafunzo
Muislamu amehimizwa kuswali swala za faradhi na za sunna, kwakuwa zinakusanya ndani yake kusujudu.
Kumebainishwa uelewa wa Maswahaba na elimu yao kuwa pepo haipatikani -baada ya huruma ya Mwenyezi Mungu- isipokuwa kwa matendo.
Kusujudu ndani ya swala ni katika sababu kubwa za kunyanyuliwa daraja, na kusamehewa madhambi.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 353) (488).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين.
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (1/ 188).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (1/ 137).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 105).
شرح النووي على مسلم، (4/ 205).
عن أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «مَنْ صَلَّى الْبَرْدَيْنِ دَخَلَ الْجَنَّةَ»
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- ya kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeswali (wakati) wa baridi mbili ataingia peponi"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amehimiza kufanya bidii katika kuswali Swala mbili za nyakati za baridi, ambazo ni sala ya Alfajiri na Alasiri, na akawabashiria kuwa mwenye kutekeleza haki zake kwa muda, na kwa jamaa na mambo mengine, basi zitakuwa ni sababu ya kuingia kwake Peponi.
Mafunzo
Fadhila ya kuhifadhi Sala ya Alfajiri na Alasiri; Kwa sababu Alfajiri ni wakati wa usingizi mzuri, na Alasiri ni wakati mtu anashughulika na kazi zake, basi atakayezihifadhi atakuwa na haki zaidi ya kuzihifadhi Swala zilizosalia.
Sala ya Alfajiri na Alasiri zimeitwa baridi mbili; Kwa sababu Swala ya Alfajiri ina ubaridi wa usiku, na Sala ya Alasiri ina ubaridi wa mchana, hata ikiwa ni katika wakati wa joto, ni nyepesi kuliko wakati wa kabla yake, au zimeitwa hivyo kwa kuzingatia kawaida ya nyakati nyingi huwa hivyo, kama ambavyo husemwa: Miezi miwili, kwa kumaanisha jua na mwezi.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 119) (574).
صحيح مسلم (1/ 440) (635).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (1/ 159).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 187).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hebu nielezeni lau kama Mto ungelikua mlangoni kwa mmoja wenu akioga humo kila siku mara tano, unasemaje kuhusu hilo, kunaweza kubaki na uchafu katika mwili wake?" Wakasema: Hautobakiza uchafu wowote, akasema: " Huu ndio mfano wa swala tano, Mwenyezi Mungu hufuta makosa kwa swala hizo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amefananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- swala tano za kila usiku na mchana katika kuondoa kwake na kufuta kwake madhambi madogo ni sawa na Mto ulioko mlangoni kwa mtu akioga humo kila siku mara tano, hautobakiza chochote katika uchafu wake.
Mafunzo
Fadhila hizi ni maalum kwa kufuta madhambi madogo, ama makubwa hayo ni lazima kuwe na toba.
Fadhila za kutekeleza swala tano na kuzihifadhi kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake na sunna zake.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 112) (528).
صحيح مسلم (1/ 462) (667).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (2/ 773).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص610).
المعجم الوسيط، (1/ 282).
النهاية في غريب الحديث والأثر، لابن الأثير (2/ 115).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com