Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hedhi Nifasi na Damu ya Ugonjwa.

Hadithi 4

hakika hilonitatizolinatokananamshipawakizazikukatika, lakini acha swala kwa kiasi cha siku ulizokuwa ukipata hedhi ndani yake, kisha oga na swali

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤمنين رضي الله عنها أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ أَبِي حُبَيْشٍ سَأَلَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَتْ: إِنِّي أُسْتَحَاضُ فَلاَ أَطْهُرُ، أَفَأَدَعُ الصَّلاَةَ؟ فَقَالَ: «لَا، إِنَّ ذَلِكِ عِرْقٌ، وَلَكِنْ دَعِي الصَّلاَةَ قَدْرَ الأَيَّامِ الَّتِي كُنْتِ تَحِيضِينَ فِيهَا، ثُمَّ اغْتَسِلِي وَصَلِّي».
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Fatma bint Abii Qubaishi alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Mimi hupatwa na hedhi ya ugonjwa na sitwahariki, je niache swala? Akasema: "Hapana, hakika hilonitatizolinatokananamshipawakizazikukatika, lakini acha swala kwa kiasi cha siku ulizokuwa ukipata hedhi ndani yake, kisha oga na swali".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Fatma bint Abii Qubaishi alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika mimi damu haikatiki kwangu na huendelea hata nje ya wakati wa hedhi, je itakuwa hukumu ya damu hiyo ni hukumu ya damu ya hedhi ili niache swala? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema kumwambia: Hiyo ni damu ya ugonjwa, nayo ni damu ya ugonjwa ambayo husababishwa na kukatika kwa mshipa katika mfuko wa uzazi, na si damu ya hedhi, Unapokuja muda wa hedhi uliokuwa ukipata hedhi ndani yake kwa mujibu wa ada yako ya mwezi kabla hujaugua, basi acha swala na swaumu na mengineyo anayozuiliwa kuyafanya mwenye hedhi wakati wa hedhi. Kinapomalizika kiwango cha muda huo, hapo utakuwa umetwaharika na hedhi, osha mahali palipo na damu, kisha osha mwili wako josho kamili kwa ajili ya kuondoa hadathi, kisha swali.

Mafunzo
  1. Uwajibu wa kuoga kwa mwanamke zinapomalizika siku za hedhi yake.
  2. Uwajibu wa kuswali kwa mwenye istihadha (Hedhi ya ugonjwa).
  3. Hedhi: Ni damu ya maumbile ambayo hutolewa na mfuko wa uzazi kupitia tupu ya mwanamke aliyevunja ungo, humpata katika siku maalum.
  4. Istihadha: Ni kutiririka kwa damu nje ya wakati wake kutoka nje ya mfuko wa uzazi na si ndani yake.
  5. Tofauti kati ya istihadha na damu ya hedhi: Nikuwa damu ya hedhi ni nyeusi nzito inaharufu mbaya, ama damu ya istihadha ni nyekundu nyepesi na haina harufu mbaya.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 72) (325). صحيح مسلم (1/ 262) (333). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص77). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 63). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص40).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nilimuuliza Aisha nikasema: Vipi kuhusu mwenye hedhi analipa swala na wala halipi swala?

عَنْ مُعَاذَةَ قَالَتْ: سَأَلْتُ عَائِشَةَ، فَقُلْتُ: مَا بَالُ الْحَائِضِ تَقْضِي الصَّوْمَ، وَلَا تَقْضِي الصَّلَاةَ؟ فَقَالَتْ: أَحَرُورِيَّةٌ أَنْتِ؟ قُلْتُ: لَسْتُ بِحَرُورِيَّةٍ، وَلَكِنِّي أَسْأَلُ. قَالَتْ: كَانَ يُصِيبُنَا ذَلِكَ، فَنُؤْمَرُ بِقَضَاءِ الصَّوْمِ، وَلَا نُؤْمَرُ بِقَضَاءِ الصَّلَاةِ.
Kutoka kwa Muadha amesema: Nilimuuliza Aisha nikasema: Vipi kuhusu mwenye hedhi analipa swala na wala halipi swala? Akasema: Hivi wewe ni mtu kutoka Haruuraa? (mji walikozusha fitina baina ya waislamu) Akasema: Hapana: Mimi si mtu kutoka Haruuraa, bali mimi ninauliza tu, akasema: Tulikuwa tukipatwa na hilo, tunaamrishwa kulipa swaumu, na wala hatuamrishwi kulipa swala.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Muadhi alimuuliza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Kwa nini mwenye hedhi analipa swaumu na wala halipi swala?. Akasema kumwambia: Hivi wewe ni katika Makhawariji (wanaotoka katika utiifu wa kiongozi wao) wa mji wa Haruuraa wanaokithirisha maswali kwa kutaka ugumu na kutia mkazo katika dini? Akasema: Mimi si mtu kutoka Haruuraa, bali mimi ninauliza tu, akasema: Tulikuwa tukipatwa na hedhi tukiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi tunaamrishwa kulipa swaumu, na wala hatuamrishiwi kulipa swala.

Mafunzo
  1. Kumkemea kila mwenye kuuliza swali la ukorofi na mjadala usio na faida.
  2. Haruuria imenasibishwa na mji ulioko karibu na Kufa (Iraq), na unaitwa "Haruuraa": kulikuwa na kundi la Makhawariji (wanaojitoa katika kumtii kiongozi wao), alimfananisha nao katika mambo yao, na wingi wa maswali yao, na ukaidi wao.
  3. Mwalimu anatakiwa kumbaini aliyemtaka kujifunza na kumpa muongozo.
  4. Kujibu kwa nukuu ni bora; kwa sababu Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu ziwe juu yake, hakujali maana aliyoikusudia muulizaji; na hii ni kwa sababu kujibu kwa hoja hukata zaidi mzozo.
  5. Kujisalimisha katika hukumu za Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, hata kama mja hatojua hekima yake.
  6. Amesema Nawawi: Maana ya kauli ya Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuwa kundi katika Makhawariji (wanaotoka katika kuwatii viongozi) humuwajibishia mwenye hedhi kulipa swala zilizompita wakati wa hedhi, jambo ambalo ni kinyume na makubaliano ya waislamu, na kiulizo hiki alichotumia Aisha kumuuliza ni kiulizo cha kumkemea mtu, yaani: Huu ni mfumo wa Haruria na ni mfumo mbaya mno.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 71) (321). صحيح مسلم (1/ 265) (335). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 68). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص81).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote

عن أُمِّ عَطِيَّةَ رَضي الله عنها، وكَانَتْ بايَعَت النبيَّ صلى الله عليه وسلم، قالت: كُنَّا لا نَعُدّ الكُدرَةَ والصُّفْرَةَ بعدَ الطُّهرِ شيئًا.
Kutoka kwa mama Atwiya radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa kampa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: "Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote".
Imepokelewa na Abu Daud kwa matamshi haya, na amepokea Bukhari bila ya kuzidisha (baada ya kutwaharika)DarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza swahaba mama Atwiya radhi za Allah ziwe juu yake kuwa wanawake katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake walikuwa hawayazingatii maji maji yanayotoka katika tupu -ambayo yanaelekea katika weusi, au katika njano- baada ya kuona twahara ya kutoka katika hedhi: kuwa ni hedhi, hawaachi swala na swaumu kwa sababu yake.

Mafunzo
  1. Maji maji yanayoshuka kutoka katika utupu wa mwanamke baada ya twahara ya hedhi hayazingatiwi hata kama yatakuwa na rangi ya kahawia au njano inayotokana na damu.
  2. Kushuka kwa maji maji ya kahawia au njano wakati wa hedhi na ada inazingatiwa kuwa ni hedhi; kwa sababu kwa wakati huo ni damu, ila tu inakuwa imechanganyikana na maji.
  3. Mwanamke haachi swala wala swaumu kwa sababu ya maji maji ya kahawia au ya njano yanayotoka baada ya twahara, bali atatawadha na ataswali.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 72) (326). سنن أبي داود (1/ 226) (307). توضيح الأحكام، للبسام (1/ 450). سُبل السلام، للصنعاني (1/ 153).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kaa kiasi cha siku ambazo ilikuwa ikidumu hedhi yako, kisha oga

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضي الله عنها أَنَّهَا قَالَتْ: إِنَّ أُمَّ حَبِيبَةَ بِنْتَ جَحْشٍ الَّتِي كَانَتْ تَحْتَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ شَكَتْ إِلَى رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم الدَّمَ، فَقَالَ لَهَا: «امْكُثِي قَدْرَ مَا كَانَتْ تَحْبِسُكِ حَيْضَتُكِ، ثُمَّ اغْتَسِلِي». فَكَانَتْ تَغْتَسِلُ عِنْدَ كُلِّ صَلَاةٍ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Hakika mama Habiba bint Jahshi aliyekuwa chini ya Abdulrahman bin Auf alilalamika kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu damu, akasema kumwambia: "Kaa kiasi cha siku ambazo ilikuwa ikidumu hedhi yako, kisha oga". Akawa akioga kila wakati wa swala.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alilalamika mmoja kati ya Masahaba wa kike kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuendelea kushuka kwa damu yake, Akamuamrisha aache kuswali kwa kiwango cha siku alizokuwa akikaa hedhi yake kabla ya kushuka jambo hili lililojitokeza kwa dharura, kisha aoge na aswali, akawa akioga kwa hiyari kwa kila swala.

Mafunzo
  1. Damu ya ugonjwa ni: Mwanamke kuendelea kutoka damu baada ya siku za hedhi yake ya kawaida kumalizika.
  2. Mwanamke mwenye damu ya ugonjwa (Istihadha) atajichukulia kuwa ana hedhi kwa kipindi ambacho hedhi yake ilikuwa ikimuijia, kabla hakijampata kilichompata katika damu ya ugonjwa.
  3. Kikipita kiwango cha siku za ada yake ya asili, hapo atazingatiwa kuwa katwaharika na hedhi -hata kama damu ya ugonjwa itaendelea kutoka- ataoga josho la hedhi.
  4. Mwenye damu ya ugonjwa (Istihadha) halazimiki kuoga kila wakati wa swala; kwa sababu kuoga kwa mama huyu -radhi za Allah ziwe juu yake- kulikuwa ni kwa jitihada zake, na lau kama ingelikuwa wajibu, angelibainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-.
  5. Mwenye damu ya ugonjwa analazimika kutawadha kila wakati wa swala; kwa sababu kutengukwa kwake udhu ni endelevu hakukatiki, na mfano wa mwanamke huyu ni sawa na yeyote mwenye kutengukwa udhu kusikoisha, kama mwenye tatizo la kutojizuia na mkojo, au kutokwa na upepo endelevu.
  6. Kuwauliza wenye elimu yale yenye kutatiza katika mambo ya dini, kiasi kwamba mwanamke huyu alilalamika kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-, na akamuuliza kuhusu kuzidi kwa damu inayomtokea.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 264) (334). توضيح الأحكام، للبسام (1/ 447). شرح النووي على مسلم، (4/ 25). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 390).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com