Hakika ilikuwa inakutosheleza kupiga kwa mikono yako hivi" Kisha akapiga kwa mikono yake miwili chini ya ardhi mpigo mmoja, kisha ukapaka mkono wa kushoto juu ya mkono wa kulia, na juu ya viganja vyake na uso wake
Alimtuma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Ammari Bin Yasiri radhi za Allah ziwe juu yake katika moja ya safari kwa baadhi ya haja zake, akapatwa na janaba kwa tendo la ndoa au kushukwa na manii kwa matamanio, na hakupata maji ili aoge, Na alikuwa hajui hukumu ya tayamam kwa ajili ya janaba, bali alikuwa anajua hukumu yake kwa hadathi ndogo, akajitahidi na akadhani kuwa kama ambavyo hufuta kwa udongo baadhi ya viungo vya udhu kwa kuondoa hadathi ndogo, akaona kuwa kutayamam kwa kuondoa janaba ni lazima aeneze udongo mwili mzima; kwa kuchukulia kipimo katika maji, akajigeuzageuza katika udogo mpaka akaueneza mwili mzima na akaswali, alipokuja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akamueleza kuhusu hilo; ili aone je yeye amepatia au amekosea? Akambainishia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- namna ya kujitwaharisha kutokana na hadathi mbili, ndogo kama haja ndogo, na hadathi kubwa kama janaba: Nako ni mtu kupiga kwa mikono yake miwili juu ya udongo mpigo mmoja, kisha afute kwa mkono wa kushoto juu ya mkono wa kulia, na juu ya viganja vyake na uso wake.
- Ulazima wa kutafuta maji kabla ya kutayamam.
- Sheria ya kutayamam kwa mwenye janaba na akawa hakupata maji.
- Kutayamam kwa hadathi kubwa, ni sawa na kutayamam kwa hadathi ndogo.
صحيح البخاري (1/ 77) (347). صحيح مسلم (1/ 280) (368). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 60). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص72). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 92).