عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ مِنْ أَعْظَمِ الجِهَادِ كَلِمَةَ عَدْلٍ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ».
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika katika Jihadi kubwa ni kusema neno la uadilifu kwa kiongozi dhalimu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri kwa sababu ya hadithi nyinginezo
Maelezo
Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa moja ya aina kubwa ya jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na yenye manufaa makubwa ni neno la uadilifu na ukweli mbele ya mtawala au mfalme dhalimu, kwa sababu ni kuifanyia kazi sheria ya kuamrisha mema na kukataza maovu, iwe kwa maneno au maandishi au vitendo, au kitu chochote kile, ili kuleta manufaa na kuzuia maovu.
Mafunzo
- Kuamrisha mema na kukataza maovu ni katika Jihadi.
- Kumnasihi kiongozi ni katika Jihadi kubwa, lakini ni lazima iwe kwa elimu na hekima na kuwa na uhakika.
- Amesema Imam Al-Khattabi: Hii imekuwa jihadi bora kabisa kwa sababu anaye pigana na adui husitasita baina ya kuwa na matumaini na khofu, hajui atashinda au atashindwa, na kiongozi ana mamlaka mkononi mwake, hivyo ikiwa atasema kweli na akamuamrisha mema atakuwa kajitia katika hatari, na kaiweka nafsi yake katika maangamivu, hivyo ikawa ni aina bora ya jihadi kwa sababu ya kushinda khofu, na imesemwa kuwa: Imekuwa ni Jihadi bora; Kwa sababu ikiwa mtawala atachukua neno lake, faida inaweza kuenea kwa idadi kubwa ya watu, na masilahi yatapatikana.
Marejeo
سنن الترمذي (4/ 45) (2174).
سنن أبي داود (6/ 400) (4344).
سنن ابن ماجه (5/ 144) (4011).
مسند أحمد (17/ 227) (11143).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 283).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 453).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 216).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَثَلُ القَائِمِ عَلَى حُدُودِ اللَّهِ وَالوَاقِعِ فِيهَا، كَمَثَلِ قَوْمٍ اسْتَهَمُوا عَلَى سَفِينَةٍ، فَأَصَابَ بَعْضُهُمْ أَعْلاَهَا وَبَعْضُهُمْ أَسْفَلَهَا، فَكَانَ الَّذِينَ فِي أَسْفَلِهَا إِذَا اسْتَقَوْا مِنَ المَاءِ مَرُّوا عَلَى مَنْ فَوْقَهُمْ، فَقَالُوا: لَوْ أَنَّا خَرَقْنَا فِي نَصِيبِنَا خَرْقًا وَلَمْ نُؤْذِ مَنْ فَوْقَنَا، فَإِنْ يَتْرُكُوهُمْ وَمَا أَرَادُوا هَلَكُوا جَمِيعًا، وَإِنْ أَخَذُوا عَلَى أَيْدِيهِمْ نَجَوْا، وَنَجَوْا جَمِيعًا».
Kutoka kwa Nuumaan bin bashiri Radhi za Allah ziwe juu yao, kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina), wakawa baadhi yao wako juu ya safina na wengine wako chini yake, na wakawa wale walioko chini yake wanapohitajia maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, wakasema: Lau kama tungetoboa katika sehemu yetu kitobo wala tusingewaudhi walioko juu yetu, ikiwa watawaacha watekeleze walilolikusudia wataangamia wote, na ikiwa watawashika na kuwazuia wataokoka na wataokoka wote".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Mtume Rehema na amani ziwe juu yake amepiga mfano wa wale wenye kusimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu, wenye msimamo katika amri ya Mwenyezi Mungu, wenye kuamrisha mema na kukataza maovu, na mfano wa wenye kutumbukia katika mipaka ya Mwenyezi Mungu wenye kuacha mema, na kufanya maovu, na athari ya hilo katika kusalimika jamii, ni sawa na mfano wa watu waliopanda boti, wakagawana nafasi nani akae juu na nani akae chini ya boti, wengine wakapata nafasi ya kukaa juu na wengine wakapata nafasi ya kukaa chini, na wakawa hawa walioko chini wanapotaka kuchota maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, Kisha wale wa chini wakasema: Lau tungeli toboa tundu mahali petu chini ili tusiwaudhi walio juu yetu, basi lau walio juu wangewaacha kufanya hivyo, basi meli ingewazamisha wote, na lau wangeliwakataza na kuwazuia, makundi yote mawili yangeokoka.
Mafunzo
- Umuhimu wa kuamrisha mema na kukataza maovu katika kuzihifadhi jamii na kusalimika kwake.
- Miongoni mwa njia ya ufundishaji ni kupiga mifano, kwa ajili ya kusogeza uelewa wa akili kwa picha ya kitu chenye kueleweka.
- Kufanya uovu kwa wazi na kuto kukemea madhara yake yanarudi katika jamii nzima.
- Kuangamia kwa jamii kunaambatana na kuwaacha waovu wakiendelea kutapakaza maovu katika Ardhi.
- Kufanya mambo kimakosa na nia ikawa njema hili halitoshi kurekebisha matendo.
- Majukumu katika jamii ya kiislamu ni ya watu wote, hayaegemezwi kwa mtu maalum.
- Kuadhibiwa kwa watu wote kwa sababu ya madhambi ya wachache, ikiwa hayatokemewa.
- Waovu hudhihirisha maovu yao kwa sura ya kheri katika jamii kama walivyo wanafiki.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 139) (2493).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 277).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص149).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 430).
كنوز رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (4/ 39).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 210).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com