Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

7- Hukumu ya kuamrisha Mema Na Kukataza Mabaya:

Hadithi 4

Hakika watu wakimuona dhalimu na wasimchukulie hatua, basi wako karibu Mwenyezi Mungu kuwaadhibu wote kwa adhabu yake

عَنْ أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقِ رضي الله عنه أَنَّهُ قَالَ: أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّكُمْ تَقْرَؤُونَ هَذِهِ الآيَةَ: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنْفُسَكُمْ لاَ يَضُرُّكُمْ مَنْ ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ}، وَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِنَّ النَّاسَ إِذَا رَأَوْا الظَّالِمَ فَلَمْ يَأْخُذُوا عَلَى يَدَيْهِ أَوْشَكَ أَنْ يَعُمَّهُمُ اللَّهُ بِعِقَابٍ مِنْهُ».
Kutoka kwa Abubakari Swiddiq, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, ya kwamba yeye alisema: Enyi watu! Hakika nyinyi mnasoma aya hii: "Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu hatokudhuruni aliyepotoka ikiwa mtaongoka", na hakika mimi nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika watu wakimuona dhalimu na wasimchukulie hatua, basi wako karibu Mwenyezi Mungu kuwaadhibu wote kwa adhabu yake."
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Anasimulia Abubakari Swiddiq, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, kuwa watu wanasoma aya hii: "Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu hatokudhuruni aliyepotoka ikiwa mtaongoka" [Maaida: 105] Na wanaielewa kuwa mtu anatakiwa ajitume kuirekebisha nafsi yake pekee, na kwamba hatodhurika baada ya hapo kwa upotofu wa wale waliopotea, na kuwa hawajaamrishwa kuamrisha mema na kukataza maovu! Basi akawajulisha kuwa haikuwa hivyo, na kwamba alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Iwapo watu watamuona dhalimu na wasimzuie na dhulma yake, na hali yakuwa wana uwezo wa kumzuia, basi Mwenyezi Mungu yuko karibu kueneza adhabu kutoka kwake kwa wote, anayefanya uovu na anayenyamaza juu yake.

Mafunzo
  1. Ni wajibu wa Waislamu kuusiana na kuamrishana mema na kukataza maovu.
  2. Adhabu ya jumla ya Mwenyezi Mungu inajumuisha dhalimu kwa udhalimu wake, na inajumuisha yule ambaye kakaa kimya na kutomkemea ikiwa ana uweza wa kukemea.
  3. Kutoa mafunzo ya jumla na kuwaelewesha jumbe za Qur’ani kwa njia sahihi.
  4. Ni lazima mtu achunge kukielewa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ili asikielewe kwa namna tofauti na vile alivyokusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  5. Uongofu haupatikani ikiwa mtu ataacha kuamrisha mema na kukataza maovu.
  6. Tafsiri sahihi ya Aya nikuwa: Shikamaneni na kuzihifadhi nafsi zenu na maasi, mtakapozihifadhi nafsi zenu hakutokudhuruni kupotea kwa aliyepotea ikiwa mtashindwa kuamrisha mema na kukataza maovu, kwa kuyaendea kwake makatazo, pale mtakapoongoka nyinyi kuyaepuka hayo.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 40) (2168). سنن أبي داود (6/ 393) (4338). السنن الكبرى للنسائي (10/ 88) (11092). سنن ابن ماجه (5/ 139) (4005). مسند أحمد (1/ 197) (16). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 286). كنوز رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (4/ 126). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 454). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 218).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mtaamrisha mema, na mtakataza mabaya; au hakika atakuwa karibu zaidi Mwenyezi Mungu kukutumieni adhabu toka kwake, kisha mtamuomba na wala hamtojibiwa

عن حذيفة بن اليمان رضي الله عنهما عن رسول الله صلى الله عليه وسلم أنه قال: «وَالَّذِي نَفسِي بِيَدِه، لَتَأْمُرُنَّ بِالمَعرُوف، وَلَتَنهَوُنَّ عَنِ المُنْكَر؛ أَو لَيُوشِكَنَّ الله أَن يَبْعَثَ عَلَيكُم عِقَاباً مِنْه، ثُمَّ تَدعُونَه فَلاَ يُسْتَجَابُ لَكُم».
Kutoka kwa Hudhaifa bin Yamani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye alisema; "Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mtaamrisha mema, na mtakataza mabaya; au hakika atakuwa karibu zaidi Mwenyezi Mungu kukutumieni adhabu toka kwake, kisha mtamuomba na wala hamtojibiwa".
Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na AhmadDarajaNi nzuri
Maelezo

Kauli yake -Rehema na Amani ziwe juu yake-"Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake" Hiki ni kiapo anaapa Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa Mwenyezi Mungu; kwasababu yeye ndiye ambaye nafsi za waja ziko mkononi mwake -Ametakasika na kutukuka-Anaziongoza akitaka, na anazipoteza akitaka, na anazifisha akitaka, na anazibakisha akitaka, hivyo nafsi zote ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu katika uongofu na upotovu, na kuzihuisha na kuzifisha na maamuzi na mipangilio katika kila kitu, kama alivyosema Mtukufu aliyetakasika-: "Na ninaapa kwa nafsi (roho) na aliyeiumba, Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake), Hivyo nafsi ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake; na kwasababu hii aliapa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, Na alikuwa mara nyingi akiapa kwa kiapo hiki: (Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake), na wakati mwingine alikuwa akisema: (Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mkononi mwake); kwasababu nafsi ya Muhammad ndio nafsi safi zaidi kuliko zote, akaapa kwa hilo; kwakuwa ni nafsi safi. Kisha akataja alichokiapia, nacho nikuwa tusimamie kuamrisha mema na kukataza maovu; au vinginevyo atufunike Mwenyezi Mungu kwa adhabu itokayo kwake, mpaka ifikie mahali tunamuomba na wala hatukubalii, Na huu ni uwazi juu umuhimu wa kuamrisha mema kama swala na zaka na kutimiza haki, na umuhimu wa kukataza mabaya kama zinaa na riba na maharamisho mengine, na hii inakuwa kwa vitendo kwa yule ambaye ana mamlaka kama baba katika nyumba yake na mgambo wenye jukumu hilo na polisi, au kwa kauli nzuri na hili ni kwa kila mtu, au kuchukia kwa moyo pamoja na kuondoka mahala palipo na uovu, na hii ni kwa yule asiyeweza kukemea kwa vitendo au kwa kauli.

Marejeo

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، سليم بن عيد الهلالي، دار ابن الجوزي، الدمام، الطبعة: الأولى 1415هـ. سنن الترمذي، محمد بن عيسى الترمذي، تحقيق وتعليق: أحمد محمد شاكر، ومحمد فؤاد عبد الباقي، وإبراهيم عطوة عوض، شركة مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي، مصر، الطبعة: الثانية، 1395هـ- 1975م. رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين، أبو زكريا محيي الدين النووي، تحقيق ماهر الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، الطبعة: الأولى 1428هـ، 2007م. رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين، أبو زكريا محيي الدين النووي، تحقيق: عصام هادي، وزارة الأوقاف والشؤون الإسلامية القطرية، دار الريان، بيروت، الطبعة: الرابعة 1428هـ. كنوز رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين برئاسة حمد بن ناصر العمار، كنوز إشبيليا، الرياض، الطبعة: الأولى 1430هـ، 2009م. شرح رياض الصالحين، محمد بن صالح العثيمين، دار الوطن، الرياض، الطبعة: 1426هـ. صحيح الجامع الصغير وزيادته، محمد ناصر الدين الألباني، المكتب الإسلامي، بيروت، الطبعة: الثالثة 1408هـ. مسند الإمام أحمد بن حنبل، أحمد بن حنبل أبو عبدالله الشيباني، تحقيق: شعيب الأرنؤوط وعادل مرشد، وآخرون، تحت إشراف: عبد الله بن عبد المحسن التركي، مؤسسة الرسالة، الطبعة: الأولى1421هـ، 2001م. نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين، مؤسسة الرسالة، بيروت، الطبعة: الرابعة عشر 1407هـ، 1987م.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yeyote miongoni mwenu atayeona jambo ovu na baya basi aliondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi kuliondoa kwa mkono wake basi aliondoe kwa ulimi wake, na ikiwa hawezi kuliondoa kwa ulimi basi na alichukie kutoka moyoni mwake, na kuchukia moyoni ni udhaifu wa imani

عن أبي سعيد الخُدْريِّ رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «‌مَنْ ‌رَأَى ‌مِنْكُمْ ‌مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أَضْعَفُ الْإِيمَانِ».
Hadithi imepokelewa na Abii Said Alkhuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Yeyote miongoni mwenu atayeona jambo ovu na baya basi aliondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi kuliondoa kwa mkono wake basi aliondoe kwa ulimi wake, na ikiwa hawezi kuliondoa kwa ulimi basi na alichukie kutoka moyoni mwake, na kuchukia moyoni ni udhaifu wa imani".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anatuamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kuuondoa uovu, na uovu ni kila alilolikataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kadiri ya uwezo, Hivyo basi ikiwa mtu atauona uovu basi ni wajibu juu yake kuuondosha kwa mkono wake ikiwa atakuwa na uwezo wa kuuondosha uovu huo. Ikiwa atashindwa kuondosha uovu kwa mkono wake basi na auondoshe kwa ulimi wake, kwa kumkataza mwenye kufanya uovu huo, na amueleze madhara ya uovu huo na amuongoze katika kheri badala ya kufanya shari hiyo. Basi ikiwa atashindwa hatua hii ya pili, basi auondoshe uovu kwa kuchukia moyoni mwake, kwa kuuchukia uovu huo, na aazimie moyoni mwake kuwa kama angekuwa na uwezo wa kuuondosha uovu huo angeuondosha, Na kuuondosha uovu kwa moyo ni katika kiwango dhaifu zaidi cha imani katika kuuondosha uovu

Mafunzo
  1. Miongoni mwa faida za hadithi hii ni kuwa hadithi hii ni msingi katika kuweka wazi hatua na taratibu za kuuondoa uovu.
  2. Maamrisho ya kwenda hatua kwa hatua katika kukataza uovu, hatua zote hizo ni kwa mujibu wa uwezo wa mtu.
  3. Kukataza uovu katika dini ni mlango mpana sana suala hilo hakuna wakulikwepa, na hulazimishwa kila muislamu kufanya hivyo kwa kadiri ya uwezo wake.
  4. Kuamrisha mema na kukataza mabaya ni katika mambo yanayofungamana na imani, na imani kwa kawaida huzidi na kupungua.
  5. Ni sharti katika kukataza uovu: kuwa na elimu ya kuwa kitendo hicho ni uovu.
  6. Ni sharti katika kuondoa uovu: Usipelekee kutokea uovu mkubwa kuliko huo.
  7. Kukataza uovu kuna taratibu zake na masharti ambayo anapaswa muislamu kujifunza.
  8. Kukataza maovu kunahitajia siasa ya kisheria, na kuwa na ujuzi na elimu.
  9. Kutokuondosha uovu kwa moyo ni dalili ya udhaifu wa imani.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 69). جامع العلوم والحكم (2/245). المعين على تفهم الأربعين (ص 393). شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 336). البحر المحيط الثجاج (2/204). فتح القوي المتين للعباد (ص 116).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kusimzuie mmoja wenu kuwaogopa watu akaache kusema haki atakapoiona au kuijua

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: «لَا يَمْنَعَنَّ رَجُلًا مِنْكُمْ مَخَافَةُ النَّاسِ أَنْ يَتَكَلَّمَ بِالْحَقِّ إِذَا رَآهُ أَوْ عَلِمَهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kusimzuie mmoja wenu kuwaogopa watu akaache kusema haki atakapoiona au kuijua".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Alihutubia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Maswahaba zake, na miongoni mwa mambo aliyowausia ni kuwa Muislamu isimzuie hofu na kuowaogopa watu na nguvu yao akaacha kusema haki au kuiamrisha atakapoiona au kuijua.

Mafunzo
  1. Himizo la kuidhihirisha haki na kutoificha kwa kuwaogopa watu.
  2. Kusema haki haimaanishi ni kutokuwa na adabu katika mfumo wa kauli zake na hekima na mawaidha mazuri ndani yake.
  3. Uwajibu wa kuondoa uovu, na kutanguliza haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko masilahi ya watu yanayopingana na hilo.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 53) (2191). سنن ابن ماجه (5/ 141) (4007). مسند أحمد (17/ 490) (11403).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com