Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

hebu chukueni katika matendo kiasi mkiwezacho, na Wallahi ninaapa, Mwenyezi Mungu hachoki mpaka mchoke

عَنِ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنين رَضيَ اللهُ عنها زَوْجَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَنَّ الْحَوْلَاءَ بِنْتَ تُوَيْتِ بْنِ حَبِيبِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ الْعُزَّى مَرَّتْ بِهَا وَعِنْدَهَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: هَذِهِ الْحَوْلَاءُ بِنْتُ تُوَيْتٍ، وَزَعَمُوا أَنَّهَا لَا تَنَامُ اللَّيْلَ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تَنَامُ اللَّيْلَ! خُذُوا مِنَ الْعَمَلِ مَا تُطِيقُونَ، فَوَاللهِ لَا يَسْأَمُ اللهُ حَتَّى تَسْأَمُوا».
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba Haulaa binti Tuwaiti bin Habib bin Asadi bin Abdil-Uzza, alipita kwake akiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikasema: Huyu hapa Haulaa binti Tuwaiti, na wanadai kuwa huwa halali usiku, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake (kwa mshangao): "Halali usiku! hebu chukueni katika matendo kiasi mkiwezacho, na Wallahi ninaapa, Mwenyezi Mungu hachoki mpaka mchoke".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa kwa mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Haulaa bin Tuwaiti radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akatoka alipoingia tu Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Aisha akasema kumwambia: Mwanamke huyu halali usiku, bali hukesha kwa kuswali. Akasema rehema na amani ziwe juu yake akipinga kijitiadhiki kwa mwanamke huyo juu ya nafsi yake: Halali usiku! Hebu shughulikeni na matendo mema kwa kiasi mnachoweza kudumu nacho, namuapa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hachoki kuwapa waja wake wema wenye kumtii thawabu na malipo kwa utiifu wao na mema yao na amali zao njema mpaka wachoke na waache kufanya amali.

Mafunzo
  1. Kukithirisha kufanya ibada kwa zaidi ya kiwango unachoweza kuhimili mwili wa mtu hupelekea katika uchovu na kuelemewa na nafsi kuziacha.
  2. Kuwa kati na kati katika utekelezaji wa ibada hupelekea kuendelea nazo na kudumu nazo.
  3. Amali ndogo yenye kudumu ni bora kuliko nyingi yenye kukatika.
  4. Amesema Nawawi: Kwa kudumu kiwango kidogo ibada huendelea kwa kuzikumbuka na kuzichunga, na kuwa na utakasifu wa nia na kumuelekea Mwenyezi Mungu, kinyume na ibada nyingi ngumu, kiasi ambacho hizi kidogo hupanda na kuongezeka na kuzidi hizi nyingi zilizokatika mara dufu.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 17) (43). صحيح مسلم (1/ 542) (785). فتح الباري شرح صحيح البخاري، لابن رجب (1/ 164). معجم اللغة العربية المعاصرة، أحمد مختار(2/ 1020). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 212).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Haki za Mwanadamu katika uislamu

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com