Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kuenea kwa dini ya uislamu.

Hadithi 3

Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake msimshirikishe yeye na chochote, na acheni wanayosema baba zenu, na anatuamrisha swala na ukweli

عن أبي سفيان صخر بن حرب رضي الله عنه قال: قال هِرَقل: فماذا يَأمُرُكُم -يعني: النبي صلى الله عليه وسلم- قال أبو سفيان: قلت: يقول: «اعبدُوا الله وَحدَه لاَ تُشرِكُوا بِهِ شَيئًا، وَاترُكُوا ما يَقُول آبَاؤُكُم، ويَأمُرُنَا بِالصَّلاَة، والصِّدق، والعَفَاف، والصِّلَة».
Kutoka kwa Abuu Sufiyan Swakhar bin Harbi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: alisema Hiraqli: Hivi anawaamrisha nini? Yaani: Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake, akasema Abuu Sufiyani nikasema: "Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake msimshirikishe yeye na chochote, na acheni wanayosema baba zenu, na anatuamrisha swala na ukweli, na kujizuia na machafu, na kuunga udugu".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Haya ni mazungumzo ya Abuu sufiyani Swakhar bin Harbi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- ambayo ni mashuhuri yeye pamoja na Hiraqli, alikuwa Abuu Sufiyani wakati huo ni mshirikina, kiasi kwamba hakusilimu ila kwa kuchelewa, ilikuwa ni kati ya sulhul Hudaibiya (mkataba wa makubaliano wa Hudaibiya) na Fat-hu Makka (kufunguliwa kwa mji wa Makka) alitoka Abuu Sufiyani akiwa pamoja na kundi la makuraishi wakielekea kwa Hiraqli katika mji wa Sham, na Hiraqli alikuwa ni mfalme wa wakristo kwa wakati ule, na alikuwa amesoma katika taurati na Injili na vitabu vilivyotangulia, na alikuwa ni mfalme mwerevu, basi aliposikia ujio wa Abuu Sufiyani na wale walio pamoja naye, nao wakitokea katika miji ya jangwani aliwaita, na akaanza kuwauliza kuhusu hali ya Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- na kuhusu nasaba (ukoo) wake, na kuhusu maswahaba zake, na jinsi gani wanavyomuheshimu, na uaminifu wake Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- basi wanapotaja kitu wanachomueleza anazidi kujua kuwa huyu ndiye Nabii aliyeelezwa katika vitabu vilivyotangulia, lakini yeye -Tunamuomba Allah atuepushe na hilo- ni mtu mwenye uchu na ufalme wake akawa hakusilimu kwa hekima alizozitaka Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ilikuwa miongoni mwa yale aliyomuuliza Abuu Sufiyani ni kumuuliza juu ya yale anayoyaamrisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamueleza kuwa yeye anawaamrisha wao wamuabudu Mwenyezi Mungu na wala wasimshirikishe yeye na chochote, basi wasiabudu zaidi ya Mwenyezi Mungu, si Malaika wala Mtume, na wala si mti wala jiwe, na wala si jua wala mwezi, na wala si kinginecho, ibada zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, na huu ndio ujumbe wa Mtume, akaja Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na yale waliyokuja nayo Mitume kabla yake, kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika. Na akisema: "Yaacheni waliyokuwa nayo baba zenu" na hii ni katika kuutangaza ukweli, yale yote yaliyokuwa kwa baba zao katika kuabudu masanamu, aliwaamrisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuyaacha, na ama yale waliyokuwa nayo baba zao katika tabia njema; basi hakuwaamrisha wayaache. Na kauli yake: "Na alikuwa akituamrisha kuswali" swala ni mawasiliano kati ya mja na Mola wake, nayo ni nguzo ya pili yenye mkazo baada ya shahada mbili, na kupitia hii anajulikana muumini na kafiri, hiyo ndiyo ahadi iliyoko kati yetu na washirikina na makafiri, kama alivyosema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Ahadi iliyoko kati yetu sisi na wao ni swala, atakayeiacha atakuwa kakufuru" Na kauli yake: "Na alikua akituamrisha ukweli" Yaani alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiuamrisha umma wake kuwa wakweli, na hii ni kama kauli yake Mtukufu: "Enyi mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu na muwe miongoni mwa wakweli", na ukweli ni tabia njema, na unagawanyika sehemu mbili: kuwa mkweli pamoja na Mwenyezi Mungu, na kuwa mkweli pamoja na waja wa Mwenyezi Mungu, na yote mawili ni katika tabia njema. Na kauli yake "Na kujizuia na machafu" Yaani kujizuia na machafu kuna aina mbili: ni kujizuia na matamanio ya tupu, na kujizuia na matamanio ya tumbo. Na ama kujizuia kwa kwanza: nako ni mtu ajizuie na yale aliyoharamishiwa kama zinaa na njia zake na vishawishi vyake. Na ama aina ya pili ya kujizuia: nayo kujizuia kutokana na matamanio ya tumbo, yaani ni kujizuia na vile vilivyoko mikononi mwa watu, na kujizuia kutowaomba, kiasi kwamba mtu hamuombi yeyote chochote; kwasababu kuomba omba ni udhalili, na muombaji mkono wake uko chini, na mtoaji mkono wake uko juu, haifai kumuomba yeyote isipokuwa kwa yale ambayo hayana budi. Ama kauli yake: "kuunga udugu": nako ni mtu kuunga yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu ayaunge katika udugu wa karibu kisha unaofuata, na ndugu wa karibu zaidi ni wazazi wawili, kwani kuwaunga wazazi wawili ni wema na ni kuwaunga, na ndugu wa karibu wana haki ya kuungwa kulingana na ukaribu wao utakavyokuwa, kaka ana haki zaidi kuliko baba mdogo, na baba mdogo ana haki zaidi kuliko baba yake mdogo na baba, na kuunga udugu kunakuwa kulingana na jinsi watu walivyozoea.

Marejeo

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي، ط1، دار ابن الجوزي، الدمام، 1415هـ. تطريز رياض الصالحين، للشيخ فيصل المبارك، ط1، تحقيق: عبد العزيز بن عبد الله آل حمد، دار العاصمة، الرياض، 1423هـ. دليل الفالحين لطرق رياض الصالحين، لمحمد علي بن محمد بن علان، ط4، اعتنى بها: خليل مأمون شيحا، دار المعرفة، بيروت، 1425هـ. رياض الصالحين للنووي، ط1، تحقيق: ماهر ياسين الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، 1428هـ. رياض الصالحين، ط4، تحقيق: عصام هادي، وزارة الأوقاف والشؤون الإسلامية القطرية، دار الريان، بيروت، 1428هـ. شرح رياض الصالحين، للشيخ ابن عثيمين، دار الوطن للنشر، الرياض، 1426هـ. صحيح البخاري، تحقيق: محمد زهير بن ناصر الناصر، ط1، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، 1422هـ. صحيح مسلم، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت. نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين، ط14، مؤسسة الرسالة، 1407هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمْ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا، فَيَكْسِرَ الصَّلِيبَ، وَيَقْتُلَ الخِنْزِيرَ، وَيَضَعَ الجِزْيَةَ، وَيَفِيضَ المَالُ حَتَّى لاَ يَقْبَلَهُ أَحَدٌ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya ukaribu wa kuteremka Issa mwana wa Mariam amani iwe juu yake ili ahukumu baina ya watu kwa uadilifu na kwa sheria ya Muhammadi. nakuwa atavunja misalaba wanayoitukuza wakristo, nakuwa Issa amani iwe juu yake ataua nguruwe, Na pia amani iwe juu yake ataweka kodi (Jizia) na atawaamrisha watu wote kuingia katika Uislamu. Nakuwa mali itaenea na hatoikubali yeyote; na hii ni kwa sababu ya wingi wake, na kwa kutosheka kila mmoja na kile anachokimiliki mkononi mwake, na kuteremka kwa baraka na heri nyingi zenye kufuatana.

Mafunzo
  1. Kumethibitishwa kuteremka kwa Issa amani iwe juu yake zama za mwisho, nakuwa tukio hilo ni katika alama za Kiyama.
  2. Sheria ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haitofutwa na sheria yoyote.
  3. Kuteremka kwa baraka katika mali zama za mwisho, na watu kutoipenda.
  4. Habari njema ya kubakia kwa dini ya Uislamu kiasi ambacho Issa amani iwe juu yake atawahukumu watu zama za mwisho.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 82) (2222)، صحيح مسلم (1/ 135) (155)، شرح النووي على مسلم (1/471)، التوضيح (14/555)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (12/ 35).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba

عَنِ ‌ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَطَبَ النَّاسَ يَوْمَ فَتْحِ مَكَّةَ، فَقَالَ: «يَا أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّ اللهَ قَدْ أَذْهَبَ عَنْكُمْ عُبِّيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ وَتَعَاظُمَهَا بِآبَائِهَا، فَالنَّاسُ رَجُلَانِ: بَرٌّ تَقِيٌّ كَرِيمٌ عَلَى اللهِ، وَفَاجِرٌ شَقِيٌّ هَيِّنٌ عَلَى اللهِ، وَالنَّاسُ بَنُو آدَمَ، وَخَلَقَ اللهُ آدَمَ مِنْ تُرَابٍ، قَالَ اللهُ: {يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ} [الحجرات: 13]».
Na kutoka kwa Ibn Omari Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake: Ya kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwahutubia watu siku ya ufunguzi wa mji wa Makka, akasema: "Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba , basi watu wako aina mbili: Mwema mchamungu mtukufu kwa Mwenyezi Mungu, na muovu mbaya dhalili kwa Mwenyezi Mungu, na watu wote ni wana wa Adam, na amemuumba Mwenyezi Mungu Adam kutokana na udongo. Amesema Mwenyezi Mungu: "Enyi watu hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanaume na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila tofauti tofauti, ili mfahamiane, hakika mbora wenu kwa Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na ana habari (za mambo yote)" [Al Hujuraat: 13].
Imepokelewa na Tirmidhi na bin HibbanDarajaSahihi
Maelezo

Aliwahutubia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- watu siku ya ufunguzi wa mji wa Makka akasema: Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu amenyanyua na akaondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga na kujiona, na kujifaharisha kwa baba zenu (nasaba), bali watu wako aina mbili: Ni ima muumini mwema, mchamungu, mtiifu, mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, huyu ni mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, hata kama hana cheo au nasaba nzuri mbele za watu. Na ima kafiri muovu, na huyu ni dhalili kwa Mwenyezi Mungu, na wala hana thamani yoyote, hata kama ana ukoo mzuri na cheo na mamlaka. Na watu wote ni watoto wa Adam, na Mwenyezi Mungu kamuumba Adam kutokana na udongo, haifai kwa kiumbe ambaye asili yake ni udongo kuwa na kiburi na kujiona yeye ni bora, na hili linasadikishwa na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi watu! hakika sisi tumekuumbeni nyinyi kutokana na mwanaume na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila ili mpate kujuana, hakika mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na ana habari (ya myafanyayo) [Alhujrat:13].

Mafunzo
  1. Katazo la kujifaharisha kwa ukoo na vyeo.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 309) (3270)، صحيح ابن حبان (9/ 137) (3828)، عون المعبود وحاشية ابن القيم (14/ 16)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص587).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com