Ameeleza Ubai bin Kaab radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba bwana mmoja katika Maanswari (watu wa Madina) alikuwa ni mtu anayeishi mbali kuliko wote kutoka ulipo Msikiti wa Mtume, na ilikuwa haimpiti swala yoyote; bali anahudhuria swala zote pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akaambiwa: Lau ungenunua punda wa kumpanda katika giza la usiku, na katika joto la Ardhi wakati wa mchana, akasema: Sipendezwi nyumba yangu kuwa karibu na msikiti, hakika mimi ninataka aniandikie Mwenyezi Mungu hatua zangu wakati wa kuja katika swala msikitini, na kurudi kwangu ninaporudi kwa watu wangu, yakafika maneno yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Hakika amekukusanyia Mwenyezi Mungu kwako yote hayo".
- Pupa kubwa ya Maswahaba juu ya kheri na kuzidisha zaidi na kuchuma malipo.
- Amesema Nawawi: Hapa kumethibitishwa thawabu katika hatua wakati wa kurudi kutoka katika swala kama zinavyopatikana katika kwenda.
- Kuelezana waislamu mambo ya heri na kuusiana wema, atakayeona ndugu yake kuwa anapatwa na tabu basi amfuate na amnasihi kuziondoa tabu hizo.
- Nyumba kuwa mbali na msikiti si udhuru wa kuacha swala ya jamaa, maadamu mtu anasikia Adhana.
صحيح مسلم (1/ 460) (663). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 162). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 199).