Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakuna kitu kinachotukuzwa zaidi kwa Allah Mtukufu kuliko dua

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اللهِ تَعَالَى مِنَ الدُّعَاءِ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kitu kinachotukuzwa zaidi kwa Allah Mtukufu kuliko dua".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna chochote katika ibada kilicho bora zaidi mbele ya Allah Mtukufu kuliko dua; kwa sababu ndani yake kuna kukiri utajiri wa Allah Mtukufu, na kukiri kushindwa kwa mja na kuhitajia kwake kutoka kwake.

Mafunzo
  1. Ubora wa dua nakuwa mwenye kumuomba Allah basi huwa kamtukuza, na amekiri kuwa Yeye ni mkwasi -Aliyetakasika- kwani Masikini haombwi, nakuwa Yeye ni Msikivu, kwani kiziwi haombwi, nakuwa Yeye ni mkarimu, kwani bahili haombwi, nakuwa yeye anahuruma, kwani mkorofi haombwi, nakuwa Yeye anaweza, kwani asiyejiweza haombwi, nakuwa Yeye yuko karibu, kwani aliyembali hasikii, na zinginezo katika sifa za utukufu na za uzuri wa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na Kutukuka-.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 385) (3370). سنن ابن ماجه (5/ 6) (3829). مسند أحمد (14/ 360) (8748). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 546). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 416). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 481). سبل السلام بشرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 707).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Fadhila za Dua.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com