Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha anayemfuata kwa ukaribu

عَنْ بَهْزِ بْنِ حَكِيمٍ عَنْ أَبِيهِ عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ: مَنْ أَبَرُّ؟ قَالَ: «أُمَّكَ، ثُمَّ أُمَّكَ، ثُمَّ أُمَّكَ، ثُمَّ أَبَاكَ، ثُمَّ الْأَقْرَبَ فَالْأَقْرَبَ».
Kutoka kwa Bahzi bin Hakim kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha anayemfuata kwa ukaribu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu muhimu zaidi kufanyiwa wema kuliko wote, na kumfanyia hisani, na kuamiliana naye vizuri, na kuishi naye vizuri, na kusuhubiana naye na kumuunga: Ni mama, na akasisitiza haki ya mama zaidi kuliko mtu mwingine, kwa kulirudia hilo mara tatu; kwa kubainisha fadhila zake kuliko watu wengine bila kupunguza chochote. Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake anayefuata katika kutendewa wema: Kisha baba, kisha ndugu wa karibu zaidi na wa karibu anayefuata, kila ndugu anavyozidi kuwa karibu basi anakuwa na haki zaidi ya kuungwa udugu kuliko ndugu wa mbali.

Mafunzo
  1. Mazungumzo haya ni katika kumtanguliza mama, kisha baba, kisha ndugu wa karibu zaidi na wa karibu anayefuata, kulingana na daraja zao katika ukaribu.
  2. Kumebainishwa nafasi ya wazazi wawili na hasa hasa mama.
  3. Amekariri katika hadithi wema kwa mama mara tatu; na hii ni kwa sababu ya ukubwa wa fadhila yake kwa watoto wake, na kwa sababu ya wingi wa matatizo anayovumilia na tabu na uzito wa ujauzito, kisha kujifungua, kisha kunyonyesha, mambo ambayo yako kwake pekee, kisha baba anashiriki katika malezi.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 453) (5139). سنن الترمذي (3/ 463) (1897). مسند أحمد (33/ 230) (20028). عون المعبود شرح سنن أبي داود، للعظيم آبادي (14/ 33). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (6/ 54). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 187). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 194).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ubora wa Kuwatendea Wema wazazi wawili:

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com