Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akimueleza kuhusu hamu yake na mapenzi yake ya jihadi na kuhama katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alikuwa huyu bwana kaacha nyuma yake wazazi wake wawili, na imekuja katika riwaya ya Abuudaudi kuwa "Walikuwa wakilia", wakihofia maisha yake, akamuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Je kuna yeyote kati ya wazazi wako wawili yuko hai?" Akasema: Ndiyo, bali wote wawili, akasema: "Na unatafuta malipo toka kwa Allah?" Akasema: Ndiyo, akasema: "Basi rudi kwao ukawachekeshe kama ulivyowaliza". Akamrudisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika lile ambalo ni bora katika haki zake, nalo ni kurudi kwa wazazi wawili na aishi nao vizuri, kwani hilo ni katika kupambana na nafsi katika kusimamia kuwahudumia na kuwaridhisha na kuwatii, kama ilivyokuja katika riwaya ya Bukhariy na Muslim: "Basi kwao wao wawili pigana jihadi". Na aliweka wazi katika hadithi nyingine kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili na kuwatii na kuwafanyia mazuri ni bora zaidi kuliko kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyokuja katika riwaya nyingine ya kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Anasema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamuuliza kuhusu amali bora, akasema: "Ni swala" Akasema: kisha nini?: Akasema: "Jihadi" akasema: Hakika mimi nina wazazi wawili, akasema: "Kuwafanyia kwako wema wazazi wawili ndiyo bora" ameitoa bin Hibbaani, Imeonyesha hadithi hii kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili ndiyo bora kuliko Jihadi, isipokuwa kama itakuwa Jihadi ni faradhi ya lazima, basi hapo itatangulizwa juu ya kuwatii wao; kwasababu ya ulazima wake.
منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، المؤلف: حمزة محمد قاسم، راجعه: الشيخ عبد القادر الأرناؤوط، عني بتصحيحه ونشره: بشير محمد عيون الناشر: مكتبة دار البيان، دمشق - الجمهورية العربية السورية، مكتبة المؤيد، الطائف - المملكة العربية السعودية،عام النشر: 1410هـ - 1990م. بهجة الناظرين، لسليم بن عيد الهلالي، دار ابن الجوزي. نزهة المتقين، د. مصطفى سيعد الخن، د. مصطفى البغا، محي الدين مستو، علي الشرجبي، محمد أمين لطفي، مؤسسة الرسالة، بيروت، الطبعة الأولى،1397هـ - 1977م، الطبعة الرابعة عشر، 1407هـ - 1987م. شرح رياض الصالحين، المؤلف: محمد بن صالح بن محمد العثيمين، الناشر: دار الوطن للنشر، الرياض، الطبعة: 1426ه. دليل الفالحين، محمد بن علان، دار الكتاب العربي. رياض الصالحين، للنووي، تحقيق: د. ماهر بن ياسين الفحل، الناشر: دار ابن كثير للطباعة والنشر والتوزيع، دمشق - بيروت، الطبعة: الأولى، 1428هـ - 2007م. صحيح البخاري، محمد بن اسماعيل البخاري، دار طوق النجاة، الطبعة: الأولى، 1422هـ. صحيح مسلم، المؤلف: مسلم بن الحجاج أبو الحسن القشيري النيسابوري، المحقق: محمد فؤاد عبد الباقي، الناشر: دار إحياء التراث العربي - بيروت.