Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: @Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi sijaacha dhambi yoyote wala maasi yoyote madogo wala makubwa isipokuwa nimeyafanya, je mimi nitakuwa ni mwenye kusamehewa? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema kumwambia: Hivi wewe hautamki neno la shahada "Ash-hadu an-laa ilaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullah? Akarudia kumwambia hivyo mara tatu, Basi akajibu: Ndiyo nashuhudia, Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akampa habari ya ubora na utukufu wa shahada mbili na namna inavyofuta makosa, na kuwa toba hufuta makosa yaliyopita.
- Utukufu wa shahada mbili na namna inavyoyashinda madhambi kwa yule atakayesema maneno hayo kwa dhati kutoka moyoni mwake.
- Uislamu hufuta makosa yaliyopita huko nyuma.
- Tauba ya kweli hufuta makosa yaliyopita huko nyuma.
- Kurudia rudia katika kujifunza ni miongoni mwa miongozo ya bwana Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
- Utukufu wa shahada mbili, na kuwa shahada mbili ni sababu ya kuepuka kukaa Motoni milele.
مسند أبي يعلى الموصلي (6/ 155) (3433)، المعجم الصغير للطبراني (2/ 201) (1025)، شعب الإيمان (5/404) (7086)، الأحاديث المختارة للضياء المقدسي (5/ 151) (1773)، غريب الحديث للخطابي (1/255)، الترغيب والترهيب (4/55)، النهاية في غريب الحديث والأثر (1/341)، الزواجر لابن حجر الهيتمي (2/961)، جامع العلوم والحكم (1/305).