Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, isipokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «مَا يُصِيبُ الْمُسْلِمَ مِنْ نَصَبٍ وَلَا وَصَبٍ وَلَا هَمٍّ وَلَا حُزْنٍ وَلَا أَذًى وَلَا غَمٍّ حَتَّى الشَّوْكَةِ يُشَاكُهَا إِلَّا كَفَّرَ اللهُ بِهَا مِنْ خَطَايَاهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, isipokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yanayomsibu muislamu katika maradhi na msongo na huzuni na misukosuko na majanga na shida mbali mbali na hofu na njaa, hata kama utakuwa ni mwiba utakaomchoma na kumuumiza, hilo kwake linakuwa ni kafara ya madhambi kwake na kifuta makosa.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake waumini na huruma yake kwao kwa kuwasamehe madhambi hata kwa madhara madogo yanayowasibu.
  2. Ni lazima kwa muislamu ataraji malipo kwa Allah kwa yale yanayomsibu, na asubiri kwa dogo na kubwa, ili iwe ni sababu ya kunyanyuliwa daraja na ni kafara ya makosa.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 114) (5641). صحيح مسلم (4/ 1992) (2572). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 489). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 242). شرح النووي على مسلم (16/ 126). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص44). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 96). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 70).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ubora wa Tauhiid.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com