Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Makusudio ya Sheria.

Hadithi 3

Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi wasemaje endapo atakuja mtu anataka kuchukua mali yangu?

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَرَأَيْتَ إِنْ جَاءَ رَجُلٌ يُرِيدُ أَخْذَ مَالِي؟ قَالَ: «فَلَا تُعْطِهِ مَالَكَ» قَالَ: أَرَأَيْتَ إِنْ قَاتَلَنِي؟ قَالَ: «قَاتِلْهُ» قَالَ: أَرَأَيْتَ إِنْ قَتَلَنِي؟ قَالَ: «فَأَنْتَ شَهِيدٌ»، قَالَ: أَرَأَيْتَ إِنْ قَتَلْتُهُ؟ قَالَ: «هُوَ فِي النَّارِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi wasemaje endapo atakuja mtu anataka kuchukua mali yangu? Akasema: "Usimpe mali yako" Akasema: Wasemaje kama akipigana nami? Akasema: "Pigana naye" Akasema: Wasemaje kama ataniuwa? Akasema: "Basi utakuwa umekufa shahidi". Akasema: Wasemaje kama nitamuuwa? Akasema: "Huyo ataingia Motoni".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wasemaje endapo atakuja mtu akataka kuchukua mali yangu? Akasema: Hutakiwi kujisalimilisha kwake na ukampatia mali yako, akasema: Wasemaje akipigana nami? Akasema: Inafaa kwako kupigana naye, akasema: Wasemaje endapo ataniuwa? Akasema: Basi wewe utakuwa shahidi, akasema: Wasemaje endapo nikimuuwa? Akasema: Basi yeye atastahiki kuadhibiwa motoni siku ya Kiyama.

Mafunzo
  1. Anasema Nawawi: Kupambana na kibaka ni wajibu bila pingamizi lolote, na katika kujitetea kwa kuuwa kuna kauli tofauti za wanachuoni katika madhehebu yetu na madhehebu wengine, na kutetea mali ni jambo linafaa na si wajibu.
  2. Hadithi ni ushahidi kuwa, elimu kwanza kabla ya matendo, kwa sababu Swahaba alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yale yanayompasa kabla ya kufanya.
  3. Inatakiwa kwenda hatua kwa hatua katika kupambana na adui kwa mawaidha au kutaka msaada kabla ya kuanza kupigana naye, na ikiwa yeye ndio ataanza kupigana naye, basi hima yake kubwa iwe ni kumzuia na si kumpiga.
  4. Damu ya muislamu na mali yake na heshima yake ni haramu kudhuriwa.
  5. Amesema Nawawi: Tambua kuwa shahidi amegawanyika sehemu tatu; Sehemu ya kwanza ni yule aliyeuliwa katika vita na makafiri kwa sababu yoyote miongoni mwa sababu za kuuawa, huyu anahukumu ya waliokufa mashahidi katika thawabu za Akhera na katika hukumu za dini, nazo nikuwa haoshwi na wala haswaliwi, na wa pili ni shahidi katika thawabu pasina hukumu za kidunia, naye ni aliyekufa kwa maradhi ya tumbo, na aliyekufa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali, na aliyeangukiwa na jengo, na aliyeuliwa kwa kutetea mali yake, na wengineo katika wale ambao hadithi sahihi zimekuja kuwaita kuwa ni mashihidi, huyu anaoshwa na anaswaliwa na Akhera atakuwa na thawabu za waliokufa shahidi, na si lazima awe na thawabu sawa na yule wa kwanza, na wa tatu ni yule aliyechukua ngawira kwa siri, na mfano wake miongoni mwa wale ambao dalili zimekuja kuwaondoa kuitwa mashahidi, endapo watauawa katika vita na makafiri, huyu ana hukumu za mashahidi katika dunia, haoshwi, na wala haswaliwi, na wala hana thawabu zao Akhera.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 124) (140). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 449). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 936). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 389).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi yaleteni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «ما نهيتكم عنه فاجتنبوه، وما أمرتكم به فأْتُوا منه ما استطعتم، فإنما أَهلَكَ الذين من قبلكم كثرةُ مسائلهم واختلافهم على أنبيائهم».
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi yaleteni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ametuelekeza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake yakwamba yeye anapotukataza kitu ni wajibu kwetu kukiepuka bila kubagua, na akituamrisha chochote ni juu yetu kukifanya kwa kadiri tuwezavyo. Kisha akatutahadharisha ili tusijekuwa kama umma zilizotangulia pindi walipokithirisha maswali juu ya Manabii wao pamoja nakwenda kwao kinyume nao, akawaadhibu Mwenyezi Mungu kwa aina mbalimbali za maangamivu na adhabu, tunatakiwa tusiwe mfano wao ili tusiangamie kama walivyoangamia.

Mafunzo
  1. Amri ya kutekeleza maamrisho, na kuyaepuka makatazo.
  2. Katazo halikuruhusu kufanya kitu chochote miongoni mwa hivyo, na amri ikawekewa sharti la kuweza; kwasababu kuacha ni jambo linawezekana na kufanya ni jambo linahitaji uwezo wa kukileta kitendo kilichoamrishwa.
  3. Katazo la kukithirisha maswali, wameyagawanya wanachuoni maswali katika sehemu mbili: Ya kwanza: Ni yale yanayokuwa katika mfumo wa kujifunza katika mambo yanayohitajika miongoni mwa mambo ya dini, haya yameamrishwa, na miongoni mwa hayo ni maswali ya maswahaba. Na ya pili: Ni yale yanayokuwa katika mfumo wa ukaidi na kulazimisha, na haya ndiyo yaliyokatazwa.
  4. Kutahadharishwa umma huu na kutokwenda kinyume na Nabii wake, kama ilivyotokea katika umma zilizokuwa kabla yake.
  5. Katazo lake linajumuisha kidogo na kingi, kwasababu haiwezi kufikia kuyaepuka makatazo ispokuwa kwa kuyaepuka yale madogo na mengi, kwa mfano: Ametukataza kula riba, katazo linajumuisha kidogo na kingi.
  6. Kuziacha sababu zote zinazopelekea katika mambo ya haramu, kwasababu kufanya hivyo ni miongoni mwa maana za kuyaepuka.
  7. Mwanadamu ana nguvu na uwezo, kwa kauli yake: "Kwa kiasi muwezavyo" ndani ya kauli hii ni jibu la madhehebu ya Jabariyya wanaosema kuwa: mwanadamu hana uwezo, kwasababu yeye amelazimishwa juu ya matendo yake, hata pale mtu anapotikisa mkono wake wakati wa mazungumzo, wanasema kutikisa mkono huku si kwa uwezo wake, bali kalazimishwa, na hakuna shaka kuwa kauli hii ni batili na inaambatana na madhara makubwa.
  8. Haitakiwi kwa mwanadamu anaposikia amri ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake aseme: Kwani hiyo ni wajibu au ni sunna? kwa kauli yake: "Lifanyeni kwa kadiri muwezavyo".
  9. Yote aliyoyaamrisha Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- au akayakataza basi hiyo ni sheria, swasawa hilo liwe ndani ya Qur'ani au lisiwemo, itafanyiwa kazi sunna ya ziyada katika Qu'r'ani iwe amri au katazo.
  10. Kukithirisha maswali ni sababu ya kuangamia, hasa hasa katika mambo ambayo haiwezekani kuyafikia, mfano kama maswala ya ghaibu kama majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake, na hali za siku ya kiyama, usikithirishe maswali ndani yake ukaangamia, ukawa ni mtu mwenye kulazimisha mambo mwenye kujikita.
  11. Umma waliotangulia waliangamia kwa kukithiri maswali yao, na waliangamia kwa kukithiri kwenda kwao kinyume na Manabii wao.
Marejeo

-التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، مطبعة دار نشر الثقافة، الإسكندرية، الطبعة: الأولى، 1380 هـ. -شرح الأربعين النووية، للشيخ ابن عثيمين، دار الثريا للنشر. -فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، دار ابن القيم، الدمام المملكة العربية السعودية، الطبعة: الأولى، 1424هـ/2003م. -الفوائد المستنبطة من الأربعين النووية، للشيخ عبد الرحمن البراك، دار التوحيد للنشر، الرياض. -شرح الأربعين النووية، للشيخ صالح آل الشيخ، دار الحجاز، الطبعة: الثانية، 1433هـ. -الأربعون النووية وتتمتها رواية ودراية، للشيخ خالد الدبيخي، ط. مدار الوطن. -الجامع في شروح الأربعين النووية، للشيخ محمد يسري، ط. دار اليسر. -صحيح البخاري، نشر: دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم ترقيم محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى، 1422هـ. -صحيح مسلم، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، نشر: دار إحياء التراث العربي – بيروت.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda ichukuliwe ruhusa yake katika kufanya yaliyo mepesi, kama vile anavyopendelea kwa waja wake kufanya mambo yake aliyowawajibishia kuyafanya

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ أَنْ تُؤْتَى رُخَصُهُ، كَمَا يُحِبُّ أَنْ تُؤْتَى عَزَائِمُهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda ichukuliwe ruhusa yake katika kufanya yaliyo mepesi, kama vile anavyopendelea kwa waja wake kufanya mambo yake aliyowawajibishia kuyafanya".
Imepokelewa na Ibnu HibanDarajaSahihi
Maelezo

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu anapenda ziendewe ruhusa zake ambazo ameziweka, ikiwemo kufanya wepesi katika hukumu na ibada, na kufanya wepesi kwenye ibada kwa aliyekalifishwa na sheria ikiwa ni kwa dharura- kama vile kupunguza swala na kuikusanya wakati wa safari. Kama ambavyo Mwenyezi Mungu anapenda yafanywe mambo yake ya wajibu, kwa sababu amri ya Mwenyezi Mungu katika kufuata ruhusa na kutekeleza wajibu yote ni sawa.

Mafunzo
  1. Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kuwa yeye Mwenyezi Mungu aliyetakasika na machafu anapenda ruhusa yake ifanyiwe kazi.
  2. Ukamilifu wa sheria hii, na kuondosha kwake uzito kwa waislamu.
Marejeo

صحيح ابن حبان (2/ 69) (354)، فيض القدير (2/292)، نيل الأوطار (3/244).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com