Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia shaka

عَنْ أَبِي مُـحَمَّدٍ الحَسَنِ بْنِ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ - سِبْطِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَرَيْحَانَتِهِ-، قَالَ: حَفِظْتُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «دَعْ مَا يَرِيبُك إلَى مَا لَا يَرِيبُكَ».
Kutoka kwa Abuu Muhammadi Al-Hasan bin Ally bin Abii Twalib mjukuu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na marashi yake (kipenzi chake), amesema: Nilihifadhi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia shaka."
Imepokelewa na Tirmidhiy na NasaaiDarajaSahihi
Maelezo

Ameamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha lile linalokutia shaka ndani yake katika kauli na matendo kuwa limekatazwa au la, je ni halali au ni haramu, na ufanye yale usiyo na shaka nayo katika yale uliyo na uhakika na uzuri wake na uhalali wake.

Mafunzo
  1. Muislamu anatakiwa kujenga mambo yake juu ya yakini na kuacha yenye kutia shaka ndani yake, na awe na utambuzi katika dini yake.
  2. Katazo la kutumbukia katika matamanio mabaya.
  3. Ukitaka utulivu na raha achana na mambo yanayokutia shaka na kuyatupilia mbali.
  4. Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, pale alipowaamrisha katika mambo ambayo ndani yake kuna raha ya moyo, na akawakataza katika yale yanayotia msongo na utata.
Marejeo

سنن النسائي (8/ 327) (5711). سنن الترمذي (4/ 286) (2518). مسند أحمد (3/ 248) (1723). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص29). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص153). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين للنووي وابن رجب (ص56).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kukinzana na Kufanya kuwa ni sahihi.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com