Kutoka kwa Abuu Saidi Sa'di bin Maaliki bin SInani Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haifai kujidhuru wala kumdhuru mwingine."
Imepokelewa na Ibnu Maajah, Daaruqutni na wengineo huku inafika kwa MtumeDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Amebainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni lazima kuzuia madhara kwa aina zake zote na sababu zake zote kwako na kwa wengine, ni haramu kwa yeyote kujiudhi mwenyewe na mwingine kwa kiwango sawa. Na ni haramu kwake kukabiliana na madhara kwa madhara; kwa sababu madhara hayaondoshwi kwa madhara, isipokuwa kama itakua katika njia ya kulipiza kisasi pasina kuvuka mipaka.
Mafunzo
Katazo la kulipiza kwa zaidi ya vile ulivyofanyiwa.
Mwenyezi Mungu hakuwaamrisha waja wake lolote lenye kuwadhuru.
Hadithi ni kanuni katika kuharamisha kujidhuru, na kudhuru kwa kauli au vitendo au kuacha.
Katika kanuni za sheria: Ni "Madhara huondoshwa", Hivyo, sheria haikubaliani na madhara, na inakataza kujidhuru.
Marejeo
سنن الدارقطني (4/ 51) (3079).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص74).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص325).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص112).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com