Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakuna kujidhuru wala kusababisha madhara, na atakayedhuru Allah naye atamdhuru, na atakayemtia mtu uzito Mwenyezi Mungu atamtia uzito naye

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «لَا ضَرَرَ وَلَا ضِرَارَ، مَنْ ضَارَّ ضَرَّهُ اللَّهُ، وَمَنْ شَاقَّ شَقَّ اللَّهُ عَلَيْهِ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kujidhuru wala kusababisha madhara, na atakayedhuru Allah naye atamdhuru, na atakayemtia mtu uzito Mwenyezi Mungu atamtia uzito naye".
Imepokelewa na Addar- AlqutniDarajaNi sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali
Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni lazima kuzuia madhara kwa aina zake zote na sababu zake zote kwako na kwa wengine,ni haramu kwa yeyote kujiudhi mwenyewe na mwingine kwa kiwango sawa. Na ni haramu kwake kukabiliana na madhara kwa madhara; kwa sababu madhara hayaondoshwi kwa madhara, isipokuwa kama itakua katika njia ya kulipiza kisasi pasina kuvuka mipaka. Kisha akabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- adhabu pale yanapotokea madhara kwa mtu mwenye kuwadhuru watu, na pale zinapotokea tabu kwa mtu mwenye kuwatia watu tabu.

Mafunzo
  1. Katazo la kulipiza kwa zaidi ya vile ulivyofanyiwa.
  2. Mwenyezi Mungu hakuwaamrisha waja wake lolote lenye kuwadhuru.
  3. Katazo la kujidhuru au kudhuru ima kwa kauli au kitendo au kuacha.
  4. Malipo hulingana na kitendo, atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakaye tia ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtia ugumu.
  5. Katika kanuni za sheria: Ni "Madhara huondoshwa", Hivyo, sheria haikubaliani na madhara, na inakataza kujidhuru.
Marejeo

سنن الدارقطني (4/ 51) (3079). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص74). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص325). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص112).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kanuni za Kifiq'hi na za Kimsingi.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com