Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hukumu ya Kisheria.

Hadithi 3

Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi

عن النُّعمان بن بَشير رضي الله عنه قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ -وَأَهْوَى النُّعْمَانُ بِإِصْبَعَيْهِ إِلَى أُذُنَيْهِ-: «إِنَّ الْحَلَالَ بَيِّنٌ وَإِنَّ الْحَرَامَ بَيِّنٌ، وَبَيْنَهُمَا مُشْتَبِهَاتٌ لَا يَعْلَمُهُنَّ كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ، فَمَنِ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ، وَمَنْ وَقَعَ فِي الشُّبُهَاتِ وَقَعَ فِي الْحَرَامِ، كَالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الْحِمَى يُوشِكُ أَنْ يَرْتَعَ فِيهِ، أَلَا وَإِنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمًى، أَلَا وَإِنَّ حِمَى اللهِ مَحَارِمُهُ، أَلَا وَإِنَّ فِي الْجَسَدِ مُضْغَةً، إِذَا صَلَحَتْ صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، وَإِذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، أَلَا وَهِيَ الْقَلْبُ».
Imepokewa Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Nuuman akashusha vidole vyake masikioni mwake-" "Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi na kati ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza, hawayajui mambo hayo wengi miongoni mwa watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza, basi atakuwa kaihifadhi dini yake na heshima yake, na atakayeingia katika mambo yenye kutatiza atakuwa kaingia katika haramu, ni kama mfano wa mchunga mifugo mwenye kuchungia kando kando ya mipaka wanahofiwa (mifugo wake) kuingia humo, tambueni na hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo yake, na tambueni kuwa katika mwili kuna kipande cha nyama, kikitengemaa mwili mzima unatengemaa, na kikiharibika, mwili mzima unaharibika, tambueni kipande hicho ni moyo."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kanuni kuu katika mambo, nakuwa zinagawanyika sehemu tatu katika sheria: Halali ya wazi, na haramu ya wazi, na mambo yenye kutatiza, hukumu yake haiko wazi upande wa uhalali na uharamu, watu wengi hawajui hukumu yake. Atakayeacha mambo hayo yenye kutatiza kwake, dini yake itasalimika kwa kuwa mbali na kuingia katika haramu, na heshima yake itasalimika kutokana na maneno ya watu, kwa yale wanayoweza kumuaibisha kwa kuyafanya kwake haya yenye kutatiza. Na asiyeyaepuka yenye kutatiza atakuwa kaitumbukiza nafsi yake, ima katika haramu, au watu kumkosea heshima yake. Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kapiga mfano ili abainishe hali ya mwenye kuyafanya mambo yenye kutatiza, nakuwa yeye ni sawa na mchunga mifugo, mwenye kuchunga karibu na ardhi ambayo kaihifadhi mwenye ardhi hiyo, inahofiwa mifugo yake kulisha katika mipaka hii kwa sababu ya ukaribu wake, na hivyo hivyo mwenye kufanya mambo yenye utata ndani yake, basi kwa kufanya hivyo anakuwa karibu na haramu na anahofiwa kutumbukia ndani yake. Na baada yake akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama (Nacho ni moyo) mwili hutengemaa kwa kutengemaa kwake, na huharibika kwa kuharibika kwake.

Mafunzo
  1. Himizo la kuacha yenye kutatiza, ambayo hukumu yake haijabainika.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 20) (52). صحيح مسلم (3/ 1219) (1599). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثا النووية (ص18). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص105). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص41). فتح الباري لابن حجر (4/ 291). شرح النووي على مسلم (11/ 28).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda ichukuliwe ruhusa yake katika kufanya yaliyo mepesi, kama vile anavyopendelea kwa waja wake kufanya mambo yake aliyowawajibishia kuyafanya

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ أَنْ تُؤْتَى رُخَصُهُ، كَمَا يُحِبُّ أَنْ تُؤْتَى عَزَائِمُهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda ichukuliwe ruhusa yake katika kufanya yaliyo mepesi, kama vile anavyopendelea kwa waja wake kufanya mambo yake aliyowawajibishia kuyafanya".
Imepokelewa na Ibnu HibanDarajaSahihi
Maelezo

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu anapenda ziendewe ruhusa zake ambazo ameziweka, ikiwemo kufanya wepesi katika hukumu na ibada, na kufanya wepesi kwenye ibada kwa aliyekalifishwa na sheria ikiwa ni kwa dharura- kama vile kupunguza swala na kuikusanya wakati wa safari. Kama ambavyo Mwenyezi Mungu anapenda yafanywe mambo yake ya wajibu, kwa sababu amri ya Mwenyezi Mungu katika kufuata ruhusa na kutekeleza wajibu yote ni sawa.

Mafunzo
  1. Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kuwa yeye Mwenyezi Mungu aliyetakasika na machafu anapenda ruhusa yake ifanyiwe kazi.
  2. Ukamilifu wa sheria hii, na kuondosha kwake uzito kwa waislamu.
Marejeo

صحيح ابن حبان (2/ 69) (354)، فيض القدير (2/292)، نيل الأوطار (3/244).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika mchamungu wenu na mwenye kumjua zaidi Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mimi

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللهُ عَنْها قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا أَمَرَهُمْ أَمَرَهُمْ مِنَ الأَعْمَالِ بِمَا يُطِيقُونَ، قَالُوا: إِنَّا لَسْنَا كَهَيْئَتِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ اللَّهَ قَدْ غَفَرَ لَكَ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ، فَيَغْضَبُ حَتَّى يُعْرَفَ الغَضَبُ فِي وَجْهِهِ، ثُمَّ يَقُولُ: «إِنَّ أَتْقَاكُمْ وَأَعْلَمَكُمْ بِاللَّهِ أَنَا».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapowaamrisha anawaamrisha katika matendo yale wanayoyaweza, wakasema: Sisi hatuna nafasi kama yako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amekusamehe yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, basi anachukia mpaka anaonekana usoni kuwa amechukia, kisha anasema: "Hakika mchamungu wenu na mwenye kumjua zaidi Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mimi".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapowaamrisha watu amali miongoni mwa amali anawaamrisha kwa jambo ambalo ni jepesi kwao na si zito, kwa kuhofia wasijekushindwa kudumu nalo, na yeye pia anafanya mfano walile alilowaamrisha katika wepesi, lakini wao walimuomba kubebeshwa magumu, kwa kudhania kwao kuwa wana haja ya kuzidisha zaidi katika amali kwa sababu yeye amenyanyuliwa daraja zaidi. Wanasema: Hakika sisi hatuko katika hali kama ya kwako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu amekusamehe yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, basi anakasirika mpaka hasira inajulikana usoni kwake, kisha anasema: Hakika mchamungu wenu zaidi na mjuzi wenu kwa Mwenyezi Mungu ni mimi, basi fanyeni yale ninayowaamrisha.

Mafunzo
  1. Amesema bin Hajari: Aliwamrisha yale mepesi kwao ili wadumu nayo kama alivyosema katika hadithi nyingine: "Amali inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni ile inayodumu".
  2. Mtu mwema hapaswi kuacha jitihada katika amali kwa kutegemea wema wake.
  3. Inafaa mtu kusimulia neema alizonazo kulingana na haja ya kufanya hivyo, ikiwa atakuwa na uhakika wa kutojigamba au kujikweza.
  4. Kilicho bora katika ibada ni kuwa kati na kati na kudumu, si kupita mpaka kunakopelekea kuacha.
  5. Amesema bin Hajari: Mja anapofikia kiwango kikubwa katika ibada na matunda yake hilo kwake linakuwa ni msukumo wa kudumu nazo, ili kuzibakisha neema, na kuzizidisha kwa kushukuru.
  6. Sheria ya kukasirika wakati wa kuvunjwa jambo la kisheria, na kumkemea mwerevu anayestahili kufahamu maana ya jambo endapo atashindwa kufahamu, ili kumchochea awe makini.
  7. Huruma ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Umma wake, na kwamba dini ni nyepesi, na sheria ni takasifu na yenye upole.
  8. Hamu kubwa ya Maswahaba katika ibada, na kutaka kwao kuzidisha kufanya kheri.
  9. Kusimama katika mipaka ya sheria katika wajibu na ruhusa, na kuamini kuwa kuchukua jepesi lenye kuendana na sheria ni bora kuliko gumu linalokwenda kinyume na sheria.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 13) (20). شرح صحيح البخاري لابن بطال (73/1). عمدة القاري شرح صحيح البخاري (1/ 166).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com