Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Madai na Ushahidi.

Hadithi 3

Yeyote atakayetoa kiapo hali yakuwa ni muongo, ili ajikatie mali ya mtu Muislamu, basi atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ وَهُوَ فِيهَا فَاجِرٌ لِيَقْتَطِعَ بِهَا مَالَ امْرِئٍ مُسْلِمٍ، لَقِيَ اللَّهَ وَهُوَ عَلَيْهِ غَضْبَانُ». قَالَ: فَقَالَ الْأَشْعَثُ: فِيَّ وَاللَّهِ كَانَ ذَلِكَ؛ كَانَ بَيْنِي وَبَيْنَ رَجُلٍ مِنَ الْيَهُودِ أَرْضٌ، فَجَحَدَنِي، فَقَدَّمْتُهُ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَلَكَ بَيِّنَةٌ؟» قُلْتُ: لَا. قَالَ: فَقَالَ لِلْيَهُودِيِّ: «احْلِفْ». قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِذَنْ يَحْلِفَ وَيَذْهَبَ بِمَالِي. فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: {إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا}. إِلَى آخِرِ الْآيَةِ.
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Yeyote atakayetoa kiapo hali yakuwa ni muongo, ili ajikatie mali ya mtu Muislamu, basi atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia". Akasema: Akasema Al-Ash'athi: Kwangu mimi Wallahi kulitokea tukio hilo; kulikuwa na Ardhi baina yangu na bwana mmoja Yahudi, akanipinga kuwa si yangu, nikampeleka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuniambia: "Je una ushahidi?" Nikasema: Hapana: Akasema kumwambia Yahudi: "Toa kiapo". Anasema: Nikasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, sasa si ataapa na atachukua mali yangu!. Akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wale wanaouza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa thamani ndogo..." mpaka mwisho wa aya.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoa kiapo kwa Mwenyezi Mungu huku muapaji akijua kuwa anaapia uongo ndani yake, ili ajipatie kwa kiapo hiki mali ya mwenzake; huyu atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia, akaeleza Ash'athi bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilisema hilo wakati ambao kulikuwa na mzozo kati yake yeye na bwana mmoja Yahudi katika umiliki wa Ardhi, wakashitakiana kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema kumwambia Ash'athi: Unatakiwa kuleta ushahidi ili kuthibitisha madai yako, ukishindwa kuuleta basi hutokuwa na haki zaidi ya kiapo cha hasimu wako mshitakiwa, Ash'athi akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, basi huyu bwana Yahudi si ataapa pasina hofu na mali yangu itapotea, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu kusadikisha hilo ndani ya Qur'ani kauli yake Mtukufu: "Hakika wale wanaouza" na wanabadilisha "ahadi ya Mwenyezi Mungu", na usia wake kwa waumini kwa kutimiza amana "na viapo vyao" na viapo vyao kwa jina lake kwa uongo "kwa thamani ndogo" kwa starehe za dunia "Hao hawana fungu lolote kwao Akhera" wala sehemu "Wala hatowasemesha Mwenyezi Mungu", kwa maneno yanayowafurahisha na kuwanufaisha, bali atawaghadhibikia, "wala hatowatazama siku ya Kiyama", mtazamo wa huruma na wema, "wala hatowatakasa" kwa kuwasifia kwa mazuri, wala hatowasafisha kwa kuwapa msamaha wa madhambi na machafu "na watakuwa na adhabu chungu" yenye kuumiza kwa sababu ya yale waliyoyafanya.

Mafunzo
  1. Uharamu wa kuhalalisha mali za watu kwa dhulma.
  2. Uzito wa haki za waislamu katika kidogo na kingi.
  3. Ushahidi kwa mwenye kudai, na kiapo kwa mlalamikiwa atakapokataa.
  4. Haki inathibiti kwa mashahidi wawili, usipopatikana ushahidi kwa mlalamikaji, basi ni lazima kwa mlalamikiwa kutoa kiapo.
  5. Uharamu wa kiapo cha (kuzama) nacho ni kiapo cha uongo ambacho muapaji anajikatia haki ya mtu mwingine, nalo ni katika madhambi makubwa, ambalo linamtia mtu katika ghadhabu za Mwenyezi Mungu Mtukufu na adhabu zake.
  6. Nasaha za hakimu wakati wa mzozo, hasa hasa wakati wa kutaka kiapo.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 121) (2416). صحيح مسلم (1/ 123) (138). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 136). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص687). فتاوى اللجنة الدائمة - اللجنة الدائمة للبحوث العلمية والإفتاء (23/ 513).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, lakini ushahidi ni kwa mwenye kudai na kiapo ni kwa mwenye kukanusha

عَن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما أنَّ رسولَ اللهِ صلي الله عليه وسلم قال: «لَو يُعطَى النّاسُ بدَعواهُم لادَّعَى رِجالٌ أموالَ قَومٍ ودِماءَهُم، ولَكِنَّ البَيِّنَةَ على المُدَّعِى، واليَمينَ على مَن أنكَرَ».
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mweyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, lakini ushahidi ni kwa mwenye kudai na kiapo ni kwa mwenye kukanusha".
Imepokelewa na AlbayhaqyDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa lau watu wangelipwa kwa msingi wa madai yao tu, bila ya ushahidi wala vielelezo, basi watu watadai mali na damu za watu wengine, lakini mwenye kudai lazima awasilishe alama na ushahidi wa kile anachodai, ikiwa hana ushahidi basi madai hayo yanawasilishwa kwa mshitakiwa, na akikanusha ni lazima aape na kuachiliwa.

Mafunzo
  1. Amesema bin Daqiq Al-Idd: Na hadithi hii ni msingi katika misingi ya utoaji wa hukumu, na ni marejeo makubwa wakati wa mzozo na ugomvi.
  2. Sheria imekuja kulinda mali za watu na damu zao zisichezewe.
  3. Hakimu asikuhumu kwa elimu yake bali arudi katika ushahidi.
  4. Yeyote atakayedai madai ambayo hayana uthibitisho yatakataliwa, iwe yanahusu haki na miamala au masuala ya imani na sayansi.
Marejeo

السنن الكبرى للبيهقي تحقيق التركي (21/ 242 - 243) (21243). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص76). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص328). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، لعبد المحسن البدر (ص114).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, lakini ushahidi ni kwa mwenye kudai na kiapo ni kwa mwenye kukanusha

عَن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما أنَّ رسولَ اللهِ صلي الله عليه وسلم قال: «لَو يُعطَى النّاسُ بدَعواهُم لادَّعَى رِجالٌ أموالَ قَومٍ ودِماءَهُم، لَكِنَّ البَيِّنَةَ على المُدَّعِى، واليَمينَ على مَن أنكَرَ».
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mweyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Laiti wangelipewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, lakini ushahidi ni kwa mwenye kudai na kiapo ni kwa mwenye kukanusha".
Imepokelewa na Baihaqiy na wengineo hivi na baadhi yake iko katika Swahihi mbiliDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa lau watu wangelipwa kwa msingi wa madai yao tu, bila ya ushahidi wala vielelezo, basi watu watadai mali na damu za watu wengine, lakini mwenye kudai lazima awasilishe alama na ushahidi wa kile anachodai, ikiwa hana ushahidi basi madai hayo yanawasilishwa kwa mshitakiwa, na akikanusha ni lazima aape na kuachiliwa.

Mafunzo
  1. Amesema bin Daqiq Al-Idd: Na hadithi hii ni msingi katika misingi ya utoaji wa hukumu, na ni marejeo makubwa wakati wa mzozo na ugomvi.
  2. Sheria imekuja kulinda mali za watu na damu zao zisichezewe.
  3. Hakimu asikuhumu kwa elimu yake bali arudi katika ushahidi.
  4. Yeyote atakayedai madai ambayo hayana uthibitisho yatakataliwa, iwe yanahusu haki na miamala au masuala ya imani na sayansi.
Marejeo

السنن الكبرى للبيهقي تحقيق التركي (21/ 242 - 243) (21243). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص76). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص328). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، لعبد المحسن البدر (ص114).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com