Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَت: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تُقْطَعُ اليَدُ فِي رُبُعِ دِينَارٍ فَصَاعِدًا».
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwizi unakatwa mkono wake kwa kuiba robo Dinari ya dhahabu, na zaidi ya hapo, na kiwango chake kinalingana na kiasi cha Gramu 1.06 ya dhahabu.

Mafunzo
  1. Wizi ni katika madhambi makubwa.
  2. Ameweka mpaka Mwenyezi Mungu Mtukufu wa adhabu ya mwizi, nayo ni kukata mkono wake, kama ilivyo katika kauli yake Mtukufu: "Na mwizi mwanaume na mwizi mwanamke basi ikateni mikono yao" [Maaida: 38], na mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake yamebainisha sharti za kukata huku.
  3. Makusudio ya mkono katika hadithi ni kukikata kiganja katika maungio yake kati yake na muundi wa mkono.
  4. Na miongoni mwa hekima katika kukata mkono wa mwizi, ni kulinda mali za watu, na kumkomesha mtu mwingine katika watu wanaofanya uadui katika mali za watu.
  5. Dinari ni uzito wa dhahabu, na inalingana kwa sasa na (Gramu 4.25) kwa kipimo cha 24; hivyo robo Dinari inalingana na gramu moja na kitu.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 160) (6789). صحيح مسلم (3/ 1312) (1684). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 125). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام، (ص665).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adhabu ya wizi.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com