Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kilichokuwa halali na Haramu katika wanyama na Ndege.

Hadithi 2

Hakika Allah na Mtume wake ameharamisha kuuza pombe, na mzoga na nguruwe na masanamu

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ عَامَ الفَتْحِ وَهُوَ بِمَكَّةَ: «إِنَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ حَرَّمَ بَيْعَ الخَمْرِ، وَالمَيْتَةِ وَالخِنْزِيرِ وَالأَصْنَامِ»، فَقِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَرَأَيْتَ شُحُومَ المَيْتَةِ، فَإِنَّهَا يُطْلَى بِهَا السُّفُنُ، وَيُدْهَنُ بِهَا الجُلُودُ، وَيَسْتَصْبِحُ بِهَا النَّاسُ؟ فَقَالَ: «لاَ، هُوَ حَرَامٌ»، ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ ذَلِكَ: «قَاتَلَ اللَّهُ اليَهُودَ إِنَّ اللَّهَ لَمَّا حَرَّمَ شُحُومَهَا جَمَلُوهُ، ثُمَّ بَاعُوهُ، فَأَكَلُوا ثَمَنَهُ».
Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yao na baba yake, yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akisema siku ya ufunguzi wa mji wa Makka, akiwa Makka: "Hakika Allah na Mtume wake ameharamisha kuuza pombe, na mzoga na nguruwe na masanamu", Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wasemaje kuhusu samli (mafuta ya wanyama), kwani hutumika kupaka boti, na hupakwa ngozi, na watu huyatumia kuwasha taa? Akasema: "Hapana, hayo ni haramu", kisha baada ya hapo akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenyezi Mungu awalaani Mayahudi, kwani Mwenyezi Mungu alipowaharamishia samli (mafuta ya wanyama) waliyayeyusha, kisha wakayauza, na wakala thamani yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Jabiri bin Abdillah Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema katika mwaka wa ufunguzi akiwa Makka: Hakika Mwenyezi Mungu na Mtume wake amekataza kuuza pombe, na mzoga na nguruwe na masanamu, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je inajuzu kwetu kuuza mafuta ya wanyama waliokufa? Kwa sababu yanatumika kupaka boti (Mitumbwi), na ngozi na watu huwasha taa zao kwayo. Akasema: Hapana, kuyauza ni haramu, kisha akasema: Mwenyezi Mungu amewalaani Mayahudi, Mwenyezi Mungu alipowaharamishia mafuta ya wanyama, waliyayeyusha, kisha wakayauza na kula thamani yake.

Mafunzo
  1. Amesema Imam Nawawi: Mzoga na pombe na nguruwe: Wamekubaliana waislamu wote kuwa ni haramu kuuza chochote katika hivi.
  2. Amesema Kadhi: Hadithi hii inamaanisha kuwa kila kisichohalali kukila na kunufaika nacho basi haifai kukiuza, na wala si halali kula thamani yake, kama ilivyo katika mafuta yaliyotajwa katika hadihi
  3. Amesema bin Hajari: Mlolongo wa hadithi inaonesha kuwa ibara ya mwanzo inaguvu zaidi kwa makusudio ya kuwa kauli yake: "Ni haramu" Yaani: Kuuza na si kunufaika.
  4. Kila ujanja unaotumika kuhalalisha haramu basi ni batili.
  5. Amesema Imam Nawawi: Wamesema wanachuoni: Na katika ujumla wa uharamu wa kuuza mzoga nikuwa ni haramu kuuza maiti ya kafiri tutakapomuuwa na makafiri wakaomba kumnunua, au kutoa fidia, na imekuja katika hadithi: Yakwamba Naufal bin Abdillah Al-Makhazuumi waislamu walimuua siku ya vita vya Khandaq, makafiri wakatoa Dirham elfu kumi ili kupewa mwili wake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi hakuzichukua, na akawapa bure.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 84) (2236). صحيح مسلم (3/ 1207) (1581). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، (ص97). فتاوى اللجنة الدائمة - المجموعة الأولى- اللجنة الدائمة للبحوث العلمية والإفتاء (22/ 506). الشرح الممتع على زاد المستقنع، لابن عثيمين (1/ 71). كشف اللثام شرح عمدة الأحكام، لمحمد السفاريني الحنبلي (4/ 557). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص479).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikataza kula kila chenye meno ya chonge katika wanyama wanaoshambulia, na kila chenye mdomo wa chonge katika ndege

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضيَ اللهُ عنهُما أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم: نَهَى عَنْ كُلِّ ذِي نَابٍ مِنَ السِّبَاعِ، وَعَنْ كُلِّ ذِي مِخْلَبٍ مِنَ الطَّيْرِ.
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake -: Alikataza kula kila chenye meno ya chonge katika wanyama wanaoshambulia, na kila chenye mdomo wa chonge katika ndege.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alikataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kula kila chenye kuwinda katika wanyama wenye kushambulia, kinachowinda kwa meno ya mbele, na akakataza kula kila ndege anayekata na kukamata kwa mdomo wake.

Mafunzo
  1. Pupa ya Uislamu juu ya vitu vizuri katika kila kitu miongoni mwa vyakula na vinywaji na vinginevyo.
  2. Asili katika vyakula ni uhalali; isipokuwa vile vilivyoelezwa na sheria kuwa ni haram.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1534) (1934). سبل السلام شرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 506). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 5). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 6). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (9/ 173). فتاوى اللجنة الدائمة - المجموعة الأولى (22/ 290).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com