Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hajui kitenganishi kati ya Sura na Sura nyingine mpaka imteremkie {Bismillahir Rahmanir Rahiim}
Anaweka wazi Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: kuwa Sura za Qur'ani tukufu zilikuwa zikiteremka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haikuwa ikijulikana kitenganishi chake wala mwisho wake mpaka imteremkie: {Bismillahir Rahmanir Rahiim} basi wakati huo ndipo hujua kuwa Sura iliyotangulia imekwisha, na hiyo Bismillahi ni mwanzo wa Sura mpya.
- Bismillah hutumika kuzitenganisha Sura, isipokuwa kati ya Suratul Anfaal na Suratu t-taubah.
سنن أبي داود (2/ 91) (788)، شرح سنن أبي داود للعباد (102/ 15)، التنوير شرح الجامع الصغير (8/503)، عون المعبود (2/353).