Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika majina yenu yanayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni Abdullah na Abdul-Rahman

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ أَحَبَّ أَسْمَائِكُمْ إِلَى اللهِ عَبْدُ اللهِ وَعَبْدُ الرَّحْمَنِ».
kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika majina yenu yanayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni Abdullah na Abdul-Rahman".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba majina yanayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni kumuita mtoto wa kiume: Abdullah, au Abdul-Rahman (Mja wa Allah au Mja wa Rahman).

Mafunzo
  1. Amesema Al-Qurtubi: Yanaunganishwa na majina haya mawili yote yanayokuwa mfano wake kama Abdul-Rahiim, na Abdul-Maliki na Abdul-Swamad, na yamekuwa pendwa kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu yanaambatana na wasifu wa wajibu kwa Mwenyezi Mungu na wasifu kwa mwanadamu na ni wajibu kwake ambao ni utumwa, kisha mja akaambatanishwa kwa Mola Mlezi kuambatanishwa halisi, yakasadikisha majina haya, na yakapata utukufu kwa kuunganishwa huku, na yakapata fadhila hii, na wamesema wengineo: Hekima ya kufupisha kwa majina mawili ni kuwa haikuwahi kutokea kuambatanishwa ndani ya Qur'ani utumwa na Mwenyezi Mungu isipokuwa majina haya mawili, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na kwamba pindi aliposimama mja wa Mwenyezi Mungu akimuomba" na akasema katika aya nyingine: "Na waja wa Al-Rahman (Mwingi wa rehema) na inaungwa mkono na kauli yake Mtukufu: "Sema muombeni Allah au muombeni Al-Rahmaan".
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1682) (2132). فتح الباري لابن حجر (10/ 570).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Hukumu za mwenye kuzaliwa- mchanga

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com