Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kunyonyesha.

Hadithi 1

Kunyonya pamoja kuna haramisha yale yanayo haramishwa na kuzaliwa pamoja

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «الرَّضَاعَةُ تُحَرِّمُ مَا تُحَرِّمُ الوِلَادَةُ».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kunyonya pamoja kuna haramisha yale yanayo haramishwa na kuzaliwa pamoja."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa inakuwa haramu kwa kunyonya sawa na uharamu wa kuzaliwa na wa nasaba kama mjomba au baba mdogo au kaka n.k. na kunyonya kuna halalisha yale yanayohalalishwa na kuzaliwa miongoni mwa hukumu.

Mafunzo
  1. Hadithi ni kanuni katika hukumu za kunyonya.
  2. Amesema bin Hajari: Kauli yake: "Kunyonya pamoja kuna haramisha yale yanayo haramishwa na kuzaliwa pamoja" Yaani: Na kuna halalisha yale yanayohalalishwa, nayo kwa ujumla ni katika yale yanayohusiana na kuharamisha ndoa na yale yanayofuata, na kuenea kwa uharamu baina mnyonyaji na watoto wa mnyonyeshaji, na kuwaweka nafasi ya ndugu wa karibu katika kufaa kuwatazama na kukaa nao faragha na kusafiri pamoja, lakini hukumu zingine za umama hazihusiani na hili kama akurithiana na uwajibu wa matumizi na kuacha huru kwa umiliki na ushahidi na akili na kuondosha kisasi.
  3. Kuthibiti kwa hukumu ya uharamu kwa kunyonya uharamu wa milele.
  4. Hadithi zingine zimeonyesha kuwa uharamu wa kunyonya unathibiti kwa minyonyo mitano inayoeleweka, na iwe ndani ya miaka miwili ya mwanzoni.
  5. Walioharamishwa kwa nasaba ni: Akina mama, na wanaingia hapo mabibi na kwenda juu wa upande wa mama au baba. Na mabinti: Na wanaingia humo mabinti wa mtoto wa kike, na mabinti wa mtoto wa kiume, na kwenda chini. Na madada: Sawa sawa wawe wa upande wa baba au mama, au wa upande wa mmoja wao. Na Shangazi wote: Na wanaingia hapo madada wote wa baba wa tumbo moja na wasiokuwa wa tumbo moja, na vile vile ndugu wote wa kike wa babu zako, na kwenda juu. Na Mama wadogo au wakubwa: Na wanaingia humo dada wote wa tumbo moja na mama na wengineo, na vile vile dada wote wa mabibi, na kwenda juu, sawa sawa mabibi wawe wa upande wa baba au wa mama. Na mabinti wa kaka na mabinti wa dada, na wanaingia humo mabinti zao na kwenda chini.
  6. Wanaoharamishwa kwa sababu ya kunyonya: Wanakuwa haramu kwa kunyonya wale wanaokuwa haramu kwa nasaba, kila mwanamke aliyeharamishwa kwa nasaba mfano wake anakuwa haramu kwa kunyonya isipokuwa mama wa kaka yake na dada wa mwanaye katika kunyonya, hawa si haramu.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 170) (2646). صحيح مسلم (2/ 1068) (1444). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص96). الأحاديث الأربعون النووية وعليها الشرح الموجز المفيد، لعبد الله المحسن (ص84).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com