Asiache mapambo na kupendeza mwanamke yeyote kwa maiti zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa mume wake atakaa miezi minne na siku kumi
Aliwakataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanawake kuacha mapambo kwa kuacha urembo kama marashi au wanja na mapambo mengine na nguo nzuri kwa ajili ya maiti, sawa sawa awe baba au kaka au mtoto au wengineo, zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa atakuwa mume ni miezi minne na siku kumi, na hatovaa katika kuacha mapambo kwa ajili ya mumewe nguo zote zelizo na urembo isipokuwa nguo yenye urembo kiasi, nayo ni nguo iliyokuwa ikitengenezwa Yemen wakati huo, hutiwa urembo kabla ya kushonwa, na wala hatopaka wanja machoni kwa ajili ya urembo wa macho, wala hatojipaka kwa harufu za marashi na nyinginezo, isipokuwa kama akioga kutokana na hedhi yake kwa kutumia kipande kidogo cha Qustwi au Adhfar, nazo ni aina mbiili maarufu za udi (anaweza kutumia udi mwingine pia) ambao lengo lake si kujipamba, umeruhusiwa kwa mwenye kuoga kutokana na hedhi, kwa ajili ya kuondoa harufu mbaya, ambayo hufuatana na athari ya damu katika tupu na si kwa ajili kujitia manukato.
- Ihdad maana yake: Ni kuacha urembo na mambo yanayochochea kumuoa, anatakiwa kuepuka mapambo yote, na marashi yote, na wanja, na aepuke nguo za mapambo.
- Katazo la mwanamke kuacha urembo kwa sababu ya maiti zaidi ya siku tatu, isipokuwa mumewe.
- Kumebainishwa nafasi ya mume kwa sababu hutakiwa kukaa eda kwa mwingine zaidi ya siku tatu.
- Kuhalalishwa kuanzia siku tatu kushuka chini, kwa ajili ya kujifariji.
- Ulazima wa mwanamke kuacha urembo kwa mumewe miezi minne na siku kumi, kama hatokuwa mjamzito, na akiwa hivyo basi mpaka atakapojifungua.
- Anahalalishiwa nguo yenye mchanganyiko wa rangi isiyokuwa na urembo, na kigezo kinachotumika kuijua hapo ni kulingana na tamaduni za jamii yake.
صحيح البخاري (7/ 60) (5342- 5343). صحيح مسلم (2/ 1127) (938). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 81). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص608).