Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Gaweni mirathi kwa wastahiki wake, itakayobakia basi mwenye kustahiki zaidi upande wa mwanaume ni wa kiume

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أَلْحِقُوا الفَرَائِضَ بِأَهْلِهَا، فَمَا بَقِيَ فَلِأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ».
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Gaweni mirathi kwa wastahiki wake, itakayobakia basi mwenye kustahiki zaidi upande wa mwanaume ni wa kiume".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wenye kusimamia ugawaji wa mirathi wazigawe kwa wastahiki wake kwa mgao wa uadilifu wa kisheria kama alivyotaka Mwenyezi Mungu Mtukufu, ataanza kwa kuwapa wale wenye fungu lililokadiriwa tayari kisheria, kulingana na mafungu yao katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, nayo ni: Theluthi mbili, na theluthi moja, na sudusu (moja ya sita) na nusu, na robo, thumunu (moja ya nane), mali itakayobakia baada ya hapo, hiyo atapewa ndugu wa karibu na maiti katika wanaume, na ndugu hao huitwa aswaba (warithi wasio na mipaka).

Mafunzo
  1. Hadithi hii ni kanuni katika ugawaji wa urithi.
  2. Nikuwa ugawaji wa mirathi huanza na wale wanaostahiki kurithi waliopangiwa viwango.
  3. Kuwa mali iliyobakia baada ya hao wenye kiwango cha kisheria ni ya ndugu wa mwanaume.
  4. Kumtanguliza ndugu wa karibu kisha anayefuata, hatakiwi kurithi ndugu wa mbali kama baba mdogo, pamoja nakuwa ndugu wa karibu wapo kama baba.
  5. Ndugu asiye na kiwango katika sheria hana haki ya kurithi endapo mali itamalizika, ikawa haikubakia chochote.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 152) (6737). صحيح مسلم (3/ 1233 - 1234) (1615). فتح الباري، لابن حجر (12/ 28). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 53). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص554). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص276).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Mtu asiyekuwa na fungu maalumu la urithi.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com